KAULI YA UPANGAJI WA MATOKEO YAMTOKEA PUANI MANARA

Haji Manara.

Hivi sasa mambo yamegeuka na huenda Haji Manara anatamani maneno haya, kama ambavyo Yanga na Azam FC wanapanga matokeo, yafutike lakini teknolojia imetunza na yanatumika kama kumbukumbu ikimkumbusha kuwa mambo yamegeukia kwake wakati huu ambao Simba ina viporo 7 vya ligi kuu soka Tanzania bara.

Akiwa kwenye moja ya mikutano ya klabu na wanahabari miaka iliyopita Manara alisema, ''Kwa kawaida timu inatakiwa kucheza mechi moja na kupumzika ndani ya saa 72 lakini bodi ya ligi inatoa maelezo mengi kitu ambacho si sawa.

Aidha Manara aliweka wazi kuwa Yanga ambayo ilikuwa na viporo 9 ilikuwa inapanga matokeo kwa kutumia mfumo wa 'Indirect' kwani kuna baadhi ya timu ambazo zilikuwa zinakaribia kushuka daraja huenda zisingekuwa na ushindani wakati ambao zitacheza na Yanga.

Hata hivyo kwa upande wa pili ambao ni Yanga na Azam FC msimu huu wao wapo kimya na hawajalalamika licha ya Simba kupumzika kwa zaidi ya saa 72 lakini imekuwa haichezi mechi zake za ligi na kuendelea na maandalizi ya michuano ya kimataifa.

Chanzo:Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post