GITEGA KUWA MJI MKUU WA BURUNDI

Bunge nchini Burundi limeidhinisha mswada wa sheria ya kuhamisha mji mkuu ya serikali kutoka Bujumbura hadi Gitega.

Bujumbura itasalia kuwa mji wa kibishara wa taifa hilo dogo katika kanda ya Afrika Masharika.

Akielezea kwa kina mpango huo waziri wa mambo ya ndani Pascal Barandagie alisema lengo la hatua hii kwanza ni kuwasongezea utawala wananchi wa mikoa mbalimbali, na kutenganisha makao makuu ya kisiasa na kiuchumi kwa kuacha mji wa Bujumbura kuwa mji wa kibiashara.


Mpango huo pia unalenga, kupunguza dhana ya watu wa mikoani kwamba Bujumbura ndio sehemu tu ya kufaulu maishani na hivyo kutoa fursa kwa mji huo kupumua kutokana na msongamano wa watu.

Serikali imetilia maanani suala la usalama ikisema kwamba Gitega ni mahali salama zaidi ikizingatiwa kuwa iko katikati ya Burundi tofauti na Bujumbura ambayo iko pembezoni na karibu nampaka na nchi jirani.

Tayari serikali ya Burundi imetangaza kuwa vikao vya baraza la mawaziri vitafanyika mjini Gitega kuanzia mwezi hu wa Januari.

Wizara tano za serikali pia zinatarajiwa kuhamia mji mkuu huo mpya wa Burundi.

Baraza la seneti linaelekea kukamilisha maandalizi yake ya kuhamia mji huo uliyo na wakaazi laki tatu.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post