TETESI ZA SOKA ULAYA JAN 15,2019

Chelsea itaomba £100 kwa Eden Hazard kujiunga na Real Madrid,
Chelsea itaomba £100m iwapo mchezaji raia wa Ubelgiji Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 28, ataiambia klabu kwamba anataka kujiunga na Real Madrid. (Telegraph)

Meneja wa Arsenal Unai Emery anaridhia kumruhusu mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil, mwenye umri wa miaka 30, kuondoka katika klabu hiyo ili kuweza kuwasajili wachezaji wawili wapya. Kwa sasa Ozil ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi Arsenal katika mkataba wenye thamani ya £350,000 kwa wiki. (Mail)

Mshambuliaji wa West Ham raia wa Austria Marko Arnautovic, mwenye umri wa miaka 29, atakamilisha uhamisho wa thamani ya £35m kwenda katika timu ya ligi kuu ya China Shanghai SIPG kabla ya mwisho wa wiki. (Sun)

Hammers itamlenga mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson, mwenye umri wa miaka 26, iwapo watamruhusu Arnautovic kuondoka mwezi huu. (Sky Sports)

Sevilla imevunjika moyo kumsajili mshambuliaji wa Chelsea raia wa Uhispania Alvaro Morata, mwenye umri wa miaka 26, kutokana na gharama yake kubwa, na baada ya kukataliwa pendekezo lao la thamani ya £40m. (Evening Standard)

Morata yu tayari kupokea kato la mapato ili kujiunga na Atletico Madrid, itakayohitaji kumuuza mchezaji mwingine ili kuweza kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid. (Marca)Alvaro Morata alijitosa katika soka ya kimataifa mnamo 2014

Wachezaji wa Manchester United wanaendelea kushinikiza meneja wa mpito Ole Gunnar Solskjaer apewe mkataba wa kudumu mwishoni mwa msimu. (Telegraph)

Solskjaer anataka kumuondoa Marouane Fellaini na huenda akamruhusu mchezaji huyo wa kiungo cha kati mwenye miaka 31 raia wa Ubelgiji aondoke kwa mkopo mwezi huu Januari. (Talksport)

Kocha huyo raia wa Norway ameshauriana na meneja wa zamani Sir Alex Ferguson kuhusu uteuzi wa timu tangu apokee mikoba kutoka kwa meneja aliyefutwa kazi Jose Mourinho. (Manchester Evening News)

Chelsea wamekubali makubaliano binafsi na mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Argentina Leandro Paredes, aliye na miaka 24, na wamewasilisha ombi la thamani ya £27m kwa Zenit St Petersburg. (Mirror)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post