SIMBA,YANGA KUTOFAUTIANA MASAA MANNE UWANJANI

Wachezaji wa Yanga na Simba kwenye mazoezi.

Klabu ya soka ya Yanga imemaliza maandalizi ya mwisho salama bila majeruhi kuelekea mchezo wake wa leo dhidi ya Stand United ambao utachezwa saa 10:00 jioni, masaa manne kabla ya mechi ya AS Vita Club na Simba.

Wakati Yanga wakicheza mchezo wa leo watakuwa wanafikisha michezo 20 ya ligi huku wapinzani wao Simba ambao saa 1:00 usiku watacheza na AS Vita Club bado wana michezo 14.

Yanga wanaongoza ligi hivi sasa wakiwa na alama 53 wakifuatiwa na Azam FC yenye alama 41 huku KMC ikiwa katika nafasi ya 3 na alama 34 na Simba wapo nafasi ya 4 wakiwa na alama 33.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527