Wednesday, January 9, 2019

BABU WA MIAKA 80 ANYOFOLEWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI NA WASIOJULIKANA KAGERA

  Malunde       Wednesday, January 9, 2019

Picha haihusiani na habari hapa chini
Mzee Laurian Kakoto (80), mkazi wa kijiji cha Ihunga kata Kishanda wilayani Muleba mkoani Kagera amefariki dunia baada ya  kukatwa sehemu zake za siri na wahusika kuondoka nazo.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa mzee huyo aliondoka nyumbani Januari 7,2018 kwenda kuhemea lakini hakurudi hadi maiti yake ilipogunduliwa na wananchi ikiwa imezikwa huku nyayo za miguu zikiwa zinaonekana juu ya kaburi, Januari 08 saa moja asubuhi.

Kamanda Malimi amesema baada ya wananchi kugundua tukio hilo walitoa taarifa polisi ambao walifika na kufukua mwili huo uliokuwa umezikwa. 

“Baada ya mzee huyu kuuawa,wahusika walichimba shimo na kumzika kwa kutanguliza kichwa chini wakabakiza miguu nje, wakati wananchi wakipita waliona nyayo za miguu ya binadamu zikiwa juu ya kaburi baada ya polisi kufika ukafukuliwa na kukutwa amechinjwa shingo na kitu chenye ncha kali huku sehemu zake za siri zikiwa zimekatwa”,amesema.

Amesema tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina kutokana na mwili huo kukutwa sehemu za siri zimekatwa na wahusika kuondoka nazo.

Kamanda huyo alisema kuwa katika eneo la tukio kulikutwa na kiroba kilichokuwa na mchele na kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini waliohusika na unyama huo.
Na Mwandishi wa Malunde1 blog - Kagera

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post