POLISI WATOA SABABU ZA TRAFIKI KUMTEMBEZEA KICHAPO DEREVA WA LORI


Jeshi la Polisi mkoani Songwe limeeleza sababu ya askari wa usalama barabarani kumshambulia dereva kwa kumpiga kuwa alitumia lugha ya matusi na kutotii amri ya kumtaka atoe ushirikiano kwa wanausalama hao ambao walikuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana na maofisa toka Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra).


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa Yusuph Sarungi amewaambia waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 14, 2019 kuwa tukio hilo lilitokea juzi Jumamosi Januari 12, 2019 saa 2:30 asubuhi katika eneo la Transforma, halmashauri ya mji wa Tunduma wilayani Momba wakati askari hao wakishirikiana na maofisa toka Sumatra wakiwa kwenye ukaguzi wa magari mbalimbali.

Amesema dereva huyo Mawazo Jairos (29) mkazi wa Mbeya aliyekuwa akiendesha gari aina ya Mistubishi Fuso lenye namba za usajili T842 AAC, baada ya kusimamishwa alianza kutoa lugha za kashifa na matusi kwa askari na maofisa wa Sumatra.

Kamanda huyo amesema Jairos aliliondoa gari bila ya kuruhusiwa kwa kupitia barabara ya vumbi hali iliyolazimu askari hao kumfuatilia na kumkamata tena katika eneo la Makambini ambapo walimzuia tena.

Sarungi amesema dereva huyo aliteremka kwenye gari kwa jazba huku akiendelea kutoa matusi na kumshambulia askari...... 
Na Stephano Simbeye, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527