Picha : SHIRIKA LA REDESO LAPANDA MITI 4000 KATA YA KILOLELI KISHAPU


Katika mapambano dhidi ya athari zitokananazo na ukataji miti kiholela ikiwa ni pamoja na hali ya ukame mkoani Shinyanga,  Shirika lisilokuwa la kiserikali la REDESO linalotekeleza mradi wa kukabiliana athari za maafa katika wilaya ya Kishapu limepanda miti zaidi ya 4000 katika kata ya kiloleli kwa lengo la kukabiliana na hali hiyo.
 Akiongea na wadau wa mazingira Januari 13,2019 kutoka kata ya Kiloleli, Meneja miradi wa shirika la REDESO Charles Bulegeya alisema mabadiliko ya tabia ya nchi yanachangiwa na shughuli za kibinaadamu ikiwemo kukata miti hovyo.

Bulegeya alisema  wanaendelea kutoa elimu ya madhara ya ukataji miti ili kuiniusuru wilaya ya Kishapu na hali  ya ukame  hivyo kwa  kushirikiana na jamii shirika hilo limepanda miti elfu 4000 katika kijiji cha Kiloleli.

“Tumeshirikisha wadau kila kitongoji ili kushiriki zoezi hili la upandaji miti kwenye vyanzo vya maji,maana chanzo hiki cha maji kiloleli kinakabiriwa na kujaa tope kwa hiyo kwa kupanda miti maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji itapunguza upoteaji wa maji” ,alisema Bulegeya. 

“Tumepanda miti zaidi ya 4000 katika kijiji hiki cha Kiloleli kwa ushirikiano wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu ambao walichangangia miti 2000 pia ushirikiano wa mgodi wa mwadui walichangia miti 1000 na taasisi ilipokea miti 1000 kutoka kwa wadau” ,aliongeza Bulegeya. 

Kwa upande wake, Kaimu afisa maliasili wilaya ya Kishapu Wilson Bigirwa, alisema halmashauri hiyo imepanga utaratibu wa kila kaya ihakikishe imepanda miti kumi katika maeneo yao na kuitunza huku akiweka wazi kuwa kufikia mwezi wanne wanatarajia kumaliza zoezi la upandaji miti wilaya nzima ya Kishapu. 

“Ndugu zangu kwa wale wote tulioshiriki katika kupanda miti tuwe walinzi wa miti yetu itapendeza kabisa kama miti yote tuliyoipanda itakuwa na kuwa mfano kwa watu wengine, na Serikali za kijiji zitunge sheria ndogondogo kuwabana wale ambao hawatakuwa sambamba na sisi”,alisema Bigirwa. 

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kiloleli wamelipongeza shirika la REDESO kwa kutekeleza mradi wa upandaji miti katika kata yao ili kukabilianan na ukame unaochangia kukosekana kwa maji na kudai kuwa wapo tayari kuwa mabalozi katika utunzaji mazingira kwa kupanda miti. 

Shirika la REDESO linatekeleza miradi mbalimbali katika mkoa wa Shinyanga ikiwa ni pamoja na kuwezesha akina mama na vijana, ubunifu na uboreshaji wa mnyororo wa thamani wa zao la mkonge kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na mradi wa tatu ni mradi wa kukabilianaa na athari za maafa.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Meneja miradi wa shirika la REDESO Charles Bulegeya akielezea juu ya umuhimu wa upandaji miti ili kukabiliana na hali ya ukame wilayani Kishapu huku akiweka wazi kuwa shirika la REDESO linatekeleza mradi kukabiliana athari za maafa katika wilaya ya Kishapu. Picha zote na Steve Kanyefu- Malunde 1 blog
Kaimu afisa maliasili wilaya ya Kishapu Wilson Bigirwa akiwaelekeza wananchi  namna bora kupanda miti.
 Wananchi wa  Kijiji cha Kiloleli wakishirikiana katika zoezi la upandaji miti.

 Mtathmini na mfuatiliaji wa mradi wa kupunguza athari za maafa Isack Jonas (kulia) akishirikiana na moja ya mwananchi wa kata ya Kiloleli katika zoezi la upandaji miti ili kukabiliana na hali ya ukame katika wilaya ya Kishapu.
 Afisa mradi wa kupunguza athari za maafa Vera Cleophas (kulia) akishiriki katika upandaji miti.
 Baadhi ya wadau walioshiriki katika upandaji miti katika kata ya Kiloleli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527