Wednesday, January 23, 2019

MGAMBO WADAKWA WAKIOMBA RUSHWA YA MKAA

  Malunde       Wednesday, January 23, 2019
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Katavi, inawashikilia askari mgambo wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, kwa tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa ya magunia matatu ya mkaa pamoja na Sh 20,000.

Wawili hao wanadaiwa kupokea rushwa hiyo kutoka kwa wananachi ili waweze kusafirisha mkaa bila kuwa na leseni wala kibali cha mamlaka husika.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi, Christopher Nakuwa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Lazaro Kambaulaya na Charles Kisauko.

Nakuwa alikuwa akitoa taarifa ya utekelezaji ya majukumu ya Takukuru mbele ya waandishi wa habari jana mjini hapa kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2018.

Katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba mwaka jana Takukuru iliendelea kutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rukwa namba 11 ya mwaka 2007.

Kipindi hicho taasisis hiyo imepokea malalamiko 18 ya vitendo vya rushwa na kufungua majalada matano ikiwemo ya migogoro ya viwanja.

Peti Siyame - Habarileo Mpanda
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post