MBAO FC WAAMUA KUMBEBA ZAHERA...WAITOA GOR MAHIA


Mbao FC

Mapema jana baada ya mchezo wa Yanga na Kariobangi Sharks kumalizika kwa Yanga kutolewa kwa kufungwa mabao 3-2, kocha Mwinyi Zahera alisema hajaumizwa na matokeo kwasababu bado kuna timu za Tanzania ambazo zinaweza kubeba taifa.

Mbao FC leo wameyabeba malengo ya Zahera kwa kushinda mechi yao ya robo fainali ya michuano ya SportPesa Cup kwa kuwatoa mabingwa watetezi Gor Mahia kwa kuwafunga kwa penalti 4-3 baada ya kutoka 1-1 katika dakika 90.

Zahera alisema ''Mimi siwezi kuumia kwasababu tumetolewa ila nawatakia Simba na Mbao FC watuwakilishe vizuri ili wazifunge AFC Leopards na Gor Mahia ili waende fainali wakachukue ubingwa ubaki Tanzania'', amesema Zahera.

Mbao FC sasa itakutana na Kariobangi Sharks iliyowatoa Yanga katika mchezo wa nusu fainali huku mshindi wa robo fainali kati ya Simba na AFC Leopards atakutana na Bandari FC ambayo nayo iliitoa Singida United.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527