RAIS MAGUFULI : HAKUNA MWANASIASA ALIYEZUIWA KUFANYA MIKUTANO..MBOWE AFANYE KWENYE JIMBO LAKE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, Freeman Mbowe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema hakuna kiongozi wa kisiasa ambaye amezuiliwa kufanya mikutano kwenye eneo lake ambalo amechaguliwa na kusema hali hiyo ndiyo demokrasia.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na viongozi wa madhebebu mbalimbali ya dini ili kujadili masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.

Akijibu swali la mchungaji Lyimo ambaye aliohudhuria hafla hiyo, Rais wa Magufuli amesema hakuna mtu aliyezuiliwa kufanya mikutano kwenye maeneo yao bali lengo ni kuhakikisha waliochaguliwa na wanapewa nafasi.

Rais amesema hakuna kiongozi aliyezuiwa kufanya mkutano katika jimbo lake bali kilichozuiwa ni kwenda kufanya mikutano katika majimbo ya wengine tena kwa fujo kwani kufanya hivyo ni sawa na askofu kutoka katika kanisa lake na kwenda kuwatukana watu msikitini jambo ambalo linaweza kuvuruga amani.

“Kama ninyi mnavyoheshimiana na sisi tunataka vyama vyetu vya siasa hata kama vipo 50 viheshimiane,” amesema.

“Nataka kuwahakikishia viongozi wa dini hakuna mtu aliyezuiliwa kufanya mkutano halali mahali alipo na bahati nzuri kwa mujibu wa sheria wanaotoa vibali ni polisi ukienda utapewa.”

“Wamefanya Dar es Salaam hapa sitaki kueleza yaliyotokea maana yapo mahakamani, wamefanya chaguzi zao ni mikutano, kwa hiyo nataka kukuhakikishia baba Mchungaji Lymo (Amani) hakuna mtu aliyezuiliwa kufanya mikutano,” amesema Rais Magufuli.

"Kama ni Mbunge wa Ubungo hakuna aliyezuiliwa, yeye ni Mbunge wa Jimbo lile Mheshimiwa Kubenea, hakuna anayemzuia Mheshimiwa Mbowe kufanya mkutano kwenye jimbo lake la hai."

"Nataka vyama yetu viige mfano mzuri wa viongozi wa dini wanavyoheshimiana na kupendana, kwa sababu jukumu langu mlinipa ni kuilinda amani ya Tanzania. Hakuna mtu aliyezuiliwa kufanya mikutano mahali pake."

Amesema anataka vyama viige mifano ya viongozi wa dini wanavyoheshimiana na kusaidiana kwa sababu moja ya jambo analozingatia ni amani.

Amesema ndiyo maana hivi sasa huwezi kumsikia Hillary Clinton akizunguka kufanya mikutano sehemu mbalimbali bali ni Donald Trump pekee kwa sababu ndiyo muda wake na atapimwa katika kipindi kilichopangwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post