MAGAIDI WASHAMBULIA HOTELI YA KIFAHARI KENYA

Milipuko na Milio ya risasi vimesikika kwenye eneo la Riverside Nairobi, Kenya ambalo linazungukwa na Ofisi mbalimbali na Hoteli  ya DusitD2 ambapo Citizen TV wametipoti kwamba inahisiwa linaweza kuwa shambulio la Kigaidi.

Mkuu wa polisi wa uchunguzi wa jinai Bw George Kinoti ni miongoni mwa maafisa wakuu wa polisi waliofika kuratibu operesheni ya kuokoa watu waliokwama ndani. 

Gazeti la Daily Nation la Kenya kupitia mtandao wake wa Twitter linaripoti kuwa maofisa wenye utaalamu wa kutegua mabomu wamewasili katika eneo la tukio. 

Gazeti hilo pia linaripoti kuwa majeruhi wa mkasa huo wanakimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta na Hospitali ya Aga Khan.

 UPDATES:
Msemaji wa kundi la kigaidi la al-Shabab ameipigia BBC simu na kudai kwamba kundi hilo limehusika "katika operesheni ambayo bado inaendelea Nairobi".

Msemaji huyo hajatoa maelezo zaidi, lakini amesema kundi hilo litatoa maelezo zaidi punde operesheni yao ikikamilika.

Wametoa maelezo zaidi na kusema "watu wetu waliingia ndani na bado wako ndani ya majengo muhimu mtaa wa Westlands, Nairobi."
Advertisement

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527