IDADI YA WALIOUAWA KENYA YAFIKIA 21,WENGINE 50 HAWAJULIKANI WALIPO

Inspekta Jenerali wa Kenya Joseph Boinnet

Idadi ya waliouawa katika shambulizi la kigaidi nchini Kenya imefikia 21, baada ya serikali ya Kenya kutangaza kuwa miili mingine 6 imepatikana kutoka katika kifusi kilicho kuwa katika eneo hilo.
Pia taarifa iliyotolewa inasema kuwa afisa polisi mmoja alifariki kutokana na majeraha wakati akipewa matibabu maalum.

Akizungumza na vyombo vya habari Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Kenya Joseph Boinnet ametoa taarifa hiyo Jumatano jioni.

Amefafanua kuwa kati ya waliouwawa kuna Wakenya 16, Muingereza moja, Mmarekani mmoja na wengine wa mataifa mbalimbali.

Hata hivyo IGP ametahadharisha vyombo vya habari kujiepusha kutoa ripoti ambazo zinaweza kuhatarisha uchunguzi ambao unaendelea baada ya shambulizi hilo.

Mapema Jumatano asubuhi Rais Uhuru Kenyatta amesema alisema kuwa watu wenye silaha waliovamia eneo la biashara la hoteli na kuuwa watu 14, “wameuwawa” baada ya takriban masaa ishirini ya mapambano ambapo mamia ya raia waliokolewa na wengine wanaokadiriwa kuwa 50 bado hawajulikani walipo.

Kikundi cha Al-Qaeda chenye mafungamano na kundi la Al-Shabaab kimedai kuhusika na shambulio hilo. Kikundi hicho kimekuwa kikilenga kuishambulia Kenya tangu ilipopeleka jeshi lake nchini Somalia Octoba 2011 kupambana na kikundi hicho cha wanajihadi.

Chanzo:Voa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527