Thursday, January 10, 2019

HUYU NDIYE WAZIRI ANAYEJIKOMBA KWA RAIS MAGUFULI 'ASEMA POVU RUKSA'

  Malunde       Thursday, January 10, 2019

Rais Magufuli (kulia) alipokuwa akiipokea ndege ya Airbus A220 - 300 Dodoma.

Akiwa tayari ameshatumikia Wizara mbili katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais Magufuli, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla maesema kuwa yupo tayari kuitwa Waziri anayejikomba kwa Rais Magufuli.

Kigwangalla ambaye ni mbunge wa Nzega Vijijini amelazimika kuweka wazi hilo wakati alipokuwa akisifia utendaji kazi wa Rais Magufuli hususani kwenye suala la kununua ndege.

''Unaweza ukasema Kigwangalla Waziri anajikomba, sawa tu! Povu ruksa!'', ni sehemu ya ujumbe wake alioundika kwenye mtandao wa Twitter.

Katika Baraza la Mawaziri la kwanza kwenye awamu ya tano chini ya Rais Magufuli, Kigwangalla aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kabla ya kupelekwa kuwa Waziri kamili wa Maliasili na Utalii Oktoba 7, 2017.

Ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 iliyopewa jina la Ngorongoro imeondoka nchini Canada jana na inatarajiwa kufika nchini kesho Januari 11, 2018 baada ya kutanguliwa na ile ya kwanza iliyopewa jina la Dodoma ambayo ilitua nchini Desemba 23, 2018.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post