Sunday, January 20, 2019

BONDIA MANNY PACQUIAO AMTWANGA BRONER

  Kanyefu       Sunday, January 20, 2019
Mwanamasumbwi, Manny Pacquiao kutoka Ufipino ameshinda pambano lake dhidi ya Mmarekani Adrien Broner kwa points (Unanimous Decision) na kufanikiwa kutetea ubingwa wake wa WBA Welterweight.

Pambano hilo lilifanyika Mjini Las Vegas, Marekani asubuhi ya kuamkia leo, Majaji wote watatu wamempa Pacquiao pointi 117-111, 116-112, 116-112.

Pacquiao (40) alimzidi Broner kwenye karibia raundi zote 12, jambo ambalo limefanya apate ushindi huo kiurahisi.

Baada ya pambano hilo, Pacquiao alimtumia salamu Bondia mwenzake Floyd Mayweather kwa kumwambia kuwa akubali warudie pambano lingine.

“Mwambieni (Mayweather) arudi ulingoni, mimi nipo tayari kupambana naye.” amesema Pacquiao ambaye mwaka 2015 alipigwa na Bondia huyo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post