ALICHOKISEMA ZITTO KABWE BAADA YA SPIKA NDUGAI KUSEMA ANAMUUMIZA SANA KICHWA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, January 19, 2019

ALICHOKISEMA ZITTO KABWE BAADA YA SPIKA NDUGAI KUSEMA ANAMUUMIZA SANA KICHWA

  Malunde       Saturday, January 19, 2019

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe amesema kuwa si kweli kwamba yeye ndiye Mbunge anayemsumbua zaidi Spika Job Ndugai kama alivyodai kwani amekuwa akifuata taratibu na kanuni bila kuvunja sheria.

Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo ametoa kauli hiyo baada ya kuulizwa kuhusu maoni yake kufuatia kauli ya Spika aliyoitoa jana akidai kuwa Zitto ni mbunge anayempa tabu kutokana na kauli zake.

"Sijui kwanini Spika amesema vile kwani mimi simpi tabu, nasimamia haki na Spika afuate kanuni tu”, amesema Zitto.Januari 17 katika mkutano wake na wanahabari, Spika Ndugai amesema amekuwa akishindwa kumfukuza bungeni mbunge huyo wa Kigoma Mjini kwa kuwa ndiye pekee anayekiwakilisha chama cha ACT- Wazalendo.

"Ni kweli Zitto Kabwe ananisumbua sana lakini, ukisema umtoe Bungeni unawaza mtu mwenyewe yuko peke yake ukimsimamisha atawakilishwa na nani?. Unamuacha tu lakini wale wengine nafukuza tu maana wako wengi akikosekana kwenye mjadala atawakilishwa na wenzake, hebu nisaidieni Zitto nimfanyeje?, alihoji Spika Ndugai.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post