WATU 900 WAUAWA CONGO

Vita vya kikabila Magharibi mwa Jamhuri ya Kidmeokrasia ya Congo vimesababisha vifo vya takriban watu 890 katika muda wa siku tatu mwezi uliopita, Umoja wa mataifa unasema.


Duru za kuaminika zinaeleza mapigano kati ya jamii za Banunu na Batende yalizuka katika vijiji vinne huko Yumbi, ofisi ya Umoja wa mataifa kuhusu haki za binaadamu inasema.

Idadi kubwa ya wakaazi wa eneo hilo inaarifiwa wameachwa bila ya makaazi.

Uchaguzi mkuu wa Desemba 30 uliahirishwa huko Yumbi kutokana na ghasia.

Mashambulio hayo yanaarifiwa kutokea kuanzia Desemba 16 hadi 18.

Raia walioachwa bila ya makaazi ni pamoja na watu 16,000 waliotafuta hifadhi kwa kuvuka mto Congo hadi katika nchi jirani ya Congo-Brazzaville, umeongeza.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post