SAKATA LA KULAZWA MAKABURINI : RC HAPI AAGIZA KATIBU WA BAVICHA AKAMATWE NA POLISI POPOTE ALIPO


 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi ameliagiza Jeshi la polisi mkoani humo kufanya uchunguzi juu ya tuhuma zilizosambaa mtandaoni zikimuhusisha na imani za kishirikina.Soma zaidi HAPA

Hapi amesema hadi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 jeshi la polisi limegundua aliyetunga uzushi huo ni Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) wilaya ya Temeke, Hilda Newton.

“Nimeagiza popote alipo huyo katibu wa Bavicha akamatwe atoe maelezo ya alichokizusha mtandaoni na athibitishe alichokiandika," amesema Hapi.

Hapi amesema amepitia akaunti ya Hilda Newton na kugundua ni tabia yake kuzusha vitu vya uongo mtandaoni.

Amesema kumtaja kwa kimo chake hajaona kama ni udhalilishaji bali alitofautisha watu waliokuwa katika picha hiyo.

"Nimemtaja kuwa ni mfupi na kweli ni mfupi ukilinganisha na mtu aliyekuwa amesimama naye katika picha niliyoiposti kumtaka akajisalimishe."

Awali baada ya kutakiwa kujisalimisha, Hilda alinukuliwa akisema kwamba hatokwenda polisi kujisalimisha kama alivyotakiwa na Hapi.


Na Berdina Majinge, Mwananchi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post