WATU WATATU WAFUNGWA JELA KWA KUMUUA MWIZI MBEYA

Watu watatu wakazi wa kata ya Kalobe jijini Mbeya wamehukumiwa kwenda jela miaka saba kila mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia ya mtu mmoja aliyekuwa akidhaniwa kuwa mwizi.

Washtakiwa Abel Kashililika (31) na wenzake wawili wamefikishwa mahakamani na kusomewa shtaka la mauaji ya bila kukusudia baada ya kushiriki kumpiga Marehemu Lewis Antony (18) aliyekuwa akituhumiwa kuwa ni mwizi pamoja na wenzake wawili katika mtaa wa Isonta.

Hukumu hiyo imetolewa na jaji wa mahakama kuu Mbeya Mary Levira.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527