DAKTARI 'MLEVI' AUA MAMA NA MTOTO WAKATI WA UPASUAJI

Daktari mmoja katika jimbo la Gujarat nchini India amekamatwa na polisi baada ya kumfanyia upasuaji mama mjamzito akiwa amelewa.

Polisi wamesema kuwa mtoto alifariki punde tu baada ya upasuaji, na mama akafuatia baada ya muda mfupi.

Kipimo cha pumzi ya mdomo baadae kilithibitisha kuwa daktari aliyefanya upasuaji alikuwa amelewa.

Hata hivyo uchunguzi bado unaendelea kubaini chanzo cha vifo hivyo kama ni uzembe ama sababu nyengine za kitabibu.

Daktari PJ Lakhani ni tabibu mwandamizi mwenye uzoefu wa kutosha na amekuwa akihudumu kwenye hospitali ya serikali ya Sonavala kwa miaka 15.

Chanzo:Bbc


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527