WANAFUNZI WAFARIKI KWA KUANGUKIWA NA UKUTA

Wanafunzi wawili wa Shule za Msingi Kijichi na Shule ya Msingi Bwawani zilizopo Mtoni Kijichi wilayani Temeke jijini Dar es Salaam wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa jengo la moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Bwawani leo Alhamisi, Desemba 6, 2018 asubuhi.

Ajali hiyo ya kuanguka kwa ukuta imetokea katika Shule ya Msingi ya Kijichi ambapo pia wanafunzi watatu wa Shule hizo wamejeruhiwa kulazwa katika Hospitali ya Temeke kwa ajili ya matibabu.

Waliokufa ni Sabra Stambuli (10) wa shule ya Bwawani na Nasri Mjenge (8) wa Shule ya Kijichi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Andrew Masatya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Endelea kufuatilia taarifa zetu kwa habari zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post