Picha : AGAPE YAFANYA BONANZA LA MICHEZO KWA WANAFUNZI KATA YA USANDA KUKOLEZA VITA DHIDI YA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI

Shirika la Agape AIDS Control Program la mjini Shinyanga, limefanya Bonanza la michezo katika shule za msingi na sekondari kata ya Usanda wilaya ya Shinyanga, lengo likiwa ni kupinga vitendo vya mimba na ndoa za utotoni ambazo zimekuwa zikikatisha ndoto za wanafunzi hivyo kutofikia malengo yao.



Bonanza hilo limefanyika leo Desemba 6, 2018 katika uwanja wa shule ya msingi Shingita kwa kukutanisha wanafunzi kutoka Shule nane za kata hiyo ya Usanda ambapo za msingi ni tano na sekondari tatuili kuwapatia wanafunzi hao elimu ya afya ya uzazi na ujinsia.

Shule za msingi zilizoshiriki bonanza hilo ni Nzagaluba, Manyada, Busanda, Shabuluba pamoja na Shingida, za Sekondari ni Samuye, Usanda na Shingita,ambazo zimecheza michezo ya mpira wa miguu kwa wavulana na wanafunzi wa kike wakicheza mpira wa pete ambapo washindi wamekabidhiwa makombe.

Akizungumza kwenye Bonanza hilo Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika hilo la Agape linalotetea haki za watoto Lucy Maganga, alisema wameamua kufanya Bonanza hilo ikiwa ni sehemu ya kuwakutanisha wanafunzi pamoja na kuwapatia elimu ya kujitambua pamoja na madhara kujiingiza kwenye mahusiano wakiwa na umri mdogo.

Alisema Bonanza hilo la michezo ni la tatu kufanyika kwenye kata hiyo ya Usanda ,mahali ambapo wanatekeleza mradi wao huo wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana, kwa kutoa elimu kwa wanafunzi juu ya madhara ya kufanya ngono za mapema.

“Mabonanza haya ya michezo kwa wanafunzi yameleta matokeo chanya kwa kupunguza tatizo la mimba mashuleni pamoja na ndoa za utotoni, ambapo katika kata hii ya Usanda mwaka jana kipindi tunaanza kutekeleza mradi wetu kulikuwa na mimba 10, lakini kwa mwaka huu zipo Nne tu, na tunatarajia mwakani kusiwepo na mimba kabisa,”alisema Maganga.

Aliwataka kutoa taarifa mapema pale wanapotongozwa ama kutaka kuozeshwa ili wahusika wapate kushugulikiwa haraka na kukomesha vitendo hivyo.

Naye mgeni Rasmi kwenye Bonanza hilo Kaimu Ofisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka aliwataka wanafunzi hao elimu ambayo wanapewa na Shirika hilo la Agape waitekeleze kwa vitendo, jambo ambalo litawasaidia kutimiza ndoto zao.

Aidha aliwataka wanafunzi hao hasa wa kike kukataa kabisa kujiingiza kwenye mahusiano wakiwa bado wadogo, na kuwashitaki wanaume ambao wamekuwa wakiwatongoza kwa wazazi wao au walimu, ili wapate kushughulikiwa na kukomesha vitendo vya kikatili dhidi yao.


Nao baadhi ya wanafunzi wa kike waliohudhuria Bonanza hilo akiwemo Kemi Ishengoma kutoka Shule ya Sekondari Shingita, walisema bonanza hilo limekuwa msaada mkubwa kwao ambapo wanafunzi wengi wameweza kujitambua tofauti na zamani, mara baada ya kupewa elimu hiyo ya afya ya uzazi na ujinsia.


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga akitoa elimu kwa wanafunzi kabla ya kuanza kwa Bonanza hilo la michezo, juu kujitambua na kuacha kujiingiza kwenye mapenzi katika umri mdogo ilikutimiza malengo yao, pamoja na kutoa taarifa kwa wanaume ambao huwatongoza ili wapate kushughulikiwa.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka akizungumza kwenye Bonanza hilo na kuwataka wanafunzi hasa wa kike, washirikiane na vyombo vya dola kutoa ushahidi mahakamani pale watuhumiwa wanapokamatwa kwa kuwapatia ujauzito kutokana na kuwarubuni ili wapate kufungwa jela na kuwafundisho kwa wengine na hatimaye kukomesha vitendo hivyo ya kikatiri dhidi yao na hatimaye kuzima ndoto zao.

Afisa elimu Kata ya Usanda Kenedy Malesa akizungumza kwenye Bonanza hilo na kulipongeza Shirika la Agape kwa kutoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa wanafunzi hali ambayo imepunguza tatizo la wanafunzi kupewa ujauzito na kuolewa ndoa za utotoni tofauti na zamani.

Mwalimu wa shule ya msingi Manyada Flora Shitegwa amepongeza mabonanza hayo ya michezo ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakichangia wanafunzi kuwa wazuri darasa kutokana na ubongo wao kuchangamka na kufikiri vizuri pamoja na kupunguza tatizo la utoro shuleni.

Mwalimu wa shule ya msingi Shabuluba Victor Komba, amesema mabonanza ya michezo yamekuwa yakisaidia wanafunzi kuwa wachangamfu pamoja na kutojiingiza kwenye makundi mabaya ambayo yatawapelekea kujiingiza kwenye mahusiano, ikiwa katika mabonanza hayo pia wanapewa elimu ya kujitambua pamoja na madhara ya kufanya mapenzi katika umri mdogo.

Mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Shingita Kemi Ishengoma ,akizungumza ambapo amesema mabonanza hayo ya michezo yanayo ratibiwa na Shirika la Agape kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la nchi Sweden Sida, yamesaidia wanafunzi wengi hasa wa kike kujitambua mara baada ya kupewa elimu ya afya ya uzazi ikiwa walikuwa hawajui madhara ya kufanya mapenzi katika umri mdogo.

Wanafunzi wakisikiliza ujumbe kuhusu elimu ya afya ya uzazi na ujinsia juu ya kupinga vitendo vya mimba mashuleni na ndoa za utotoni ili wapate kutimiza ndoto zao.

Wanafunzi wakiendelea kusikiliza nasaha kutoka kwa viongozi wa Serikali na Shirika la Agape juu ya kujitambua pamoja na kutoa taarifa pale wanapotongozwa ama kutaka kuozeshwa ndoa za utoto, pamoja na wavulana kuacha kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wenzao.

Wanafunzi wakiendelea kusikiliza nasaha za kupinga vitendo vya kikatili dhidi yao bali wakiona mwanaume anawazengea kutaka kumtongoza wapige kelele ili wapate msaada pamoja na kuacha kwenda kwenye maeneo hatarishi ili kuepuka ubakaji.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka akifungua Bonanza la michezo kwa shule za msingi na sekondari katika kata ya Usanda wilayani humo.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka, akiwapatia mikono wanafunzi tayari kwa kucheza mpira wa miguu na kuwataka wacheze mpira huo kwa amani bila ya kuumizana.

Mpira ukiendelea kuchezwa kati ya shule ya msingi Nzagaluba wenye Jezi Nyekundu , na Shabuluba wenye Nyeusi na michirizi ya njano ambao ndiyo waliibuka washindi kwa mabao mawili yaliyofungwa na Elias Paulo kipindi cha kwanza dakika ya 25 na kipindi cha Pili dakika ya 27.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka, akizungumza na wanafunzi wa kike kabla ya kufungua mchezo wa mpira wa pete na kuwataka wajitambue na kutojiingiza kwenye mapenzi katika umri mdogo ili wapate kutimiza malengo yao, pamoja na kukataa kuozeshwa ndoa za utotoni.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka, akifungua mchezo wa mpira wa Pete katika bonanza hilo la michezo Kata ya Usanda wilayani humo.

Mpira wa Pete ukiendelea kuchezwa Kati ya Shule ya Sekondari Usanda wenye Jezi za Kijani na Samuye wenye Jezi Nyekundu ambao waliibuka kwa kupata magoli 13 kwa Sita.

Wakati Bonaza likiendelea Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Shingita, kujikita kwenye masomo yao na kuachana na mapenzi katika umri mdogo ambayo yatazima ndoto zao.

Mwalimu wa michezo kutoka shule ya msingi Shabuluba Victor Komba akimpatia huduma ya kwanza mwanafunzi Faustine Peter ambaye aliumia goti .

Mpira wa Pete ukiendelea kati ya Shule ya Msingi Nzagaluba wenye jezi za kijani ambao walipata magoli 24 dhini ya wenzao Shabuluba ambao walipata magoli (Seti) Tano.

Wanafunzi wakitoa burudani wakati mpira ukiwa kwenye mapumziko.

Burudani zikiendelea kutolewa.

Burudani zikiendelea kutolewa kwenye Bonanza hilo.

Mpira wa miguu ukiendelea kuchezwa kati ya Shule ya Sekondari sekondari Samuye wenye Jezi Nyeusi ambao walipata Magoli Matano dhidi ya Usanda ambao waipata goli Moja lilofungwa na Rashidi Paulo dakika ya 29 kipindi cha pili, huku magoli ya samuye yakifungwa na Steven Juma dakika ya 3 kipindi cha kwanza, goli la Pili likifungwa na Jumanne Emmanueli dakika ya 39, ambapo kipindi cha Pili Masumbuko Richard alifunga magoli yote matatu na kisha kuondoka na mpira.

Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga akipanga makombe tayari kwa kupewa washindi.

Walimu wa michezo katika shule za msingi na Sekondari kata ya Usanda wakiwa kwenye bonanza hilo kushuhudia washindi wakipewa makombe yao.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka, akikabidhi Kombe kwa washindi wa kwanza wa mpira wa Pete kutoka Shule ya msingi Nzagaluba.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka, akikabidhi Kombe kwa washindi wa Pili wa mpira wa Pete kutoka Shule ya msingi Manyada.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka, akikabidhi Kombe kwa washindi wa kwanza wa mpira wa miguu kutoka Shule ya msingi Shabuluba.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka, akikabidhi Kombe kwa washindi wa Pili wa mpira wa miguu kutoka Shule ya msingi Nzagaluba.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka, akikabidhi Kombe kwa washindi wa kwanza wa mpira wa Pete kutoka Shule ya Sekondari Samuye.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka, akikabidhi Kombe kwa washindi wa Pili wa mpira wa Pete kutoka Shule ya Sekondari Shingita.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka, akikabidhi Kombe kwa washindi wa Kwanza wa mpira wa miguu kutoka Shule ya Sekondari Samuye.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka, akikabidhi Kombe kwa washindi wa Pili wa mpira wa miguu kutoka Shule ya Sekondari Shingita.

Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka, akizungumza na wanafunzi mara baada ya kumaliza bonanza hilo na kuwataka wasiwe wepesi wa kurubunika na wanaume bali wawe na misimamo na wajasiri kukataa kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo.

Washindi wa kwanza wa mpira wa miguu kutoka shule ya msingi Shabuluba wakipiga picha ya pamoja na Ofisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka pamoja na maofisa kutoka Shirika la Agape linalotetea haki za watoto mkoani Shinyanga.

Washindi wa kwanza wa mpira wa miguu kutoka shule ya Sekondari Samuye wakipiga picha ya pamoja na Ofisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka pamoja na maofisa kutoka Shirika la Agape linalotetea haki za watoto mkoani Shinyanga.

Washindi wa kwanza wa mpira wa Pete kutoka shule ya Sekondari Samuye wakipiga picha ya pamoja na Ofisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mary Maka pamoja na maofisa kutoka Shirika la Agape linalotetea haki za watoto mkoani Shinyanga.

Picha  zote na Marco Maduhu- Malunde1 Blog.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527