TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA JUMAPILI DEC 16,2018


Manchester United wanataka kumuuza kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, 25 mwezi Januari. (Sunday Mirror)

Meneja wa United Jose Mourinho anasema hajui ikiwa klabu hiyo inamuunga mkono mwezi Januari wakati wa kununua wachezaji. (Observer)

Chelsea wana matumaijni ya kufikia makubaliano na Borussia Dortmund kwa kiungo wa kati wa miaka 20 raia wa Marekani Christian Pulisic, na kuzua wasiwasi kuhusu hatma ya Muingereza wa kikosi cha chini ya miaka 19 Wing'a Callum Hudson-Odoi ambaye anawindwa na RB Leipzig na Monaco, 18. (Mail on Sunday)Andreas Christensen

Barcelona wametoa ofa kwa baki wa Chelsea mwenye miaka 22 raia wa Denmark Andreas Christensen. (Sport - in Spanish)

Lakini kocha mkuu wa Barcelona Ernesto Valverde anasema hana ni ya kumsaini beki mpya mwezi Januari. (Goal)

Arsenal wamepewa ofa ya mchezaji wa Barcelona mwenye maiaka 24 raia wa Uhispania Denis Suarez kwa pauni milioni 14 mwezi Junuari. (Sun on Sunday)Denis Suarez

West Ham wanataka kumchukua kiungo wa kati wa Manchester United raia wa Brazil Andreas Pereira, 22, kwa mkopo mwezi Januari. (Sunday Mirror)

Everton wanataka kumsaini mshambuliaji wa RB Leipzig Jean-Kevin Augustin, 21, lakini watahitaji kulipa pauni milioni 38 kwa Mfaransa huyo. (Sun on Sunday)

Kiungo wa kati wa Southampton raia wa Ireland Kaskazini Steven Davis, 33, anaweza kurudi Rangers mwezi ujao baada ya kuwekwa kwenye kikosi cha kwanz mara mbili tu msimu huu. (Mail on Sunday)Cristian Pavon

Arsenal wanamtaka mchezaji wa Boca Juniors mwenye miaka 22 raia wa Argentina Cristian Pavon - lakini atagharimu dola milioni 40. (Sun on Sunday)

Wakati huo huo Arsenal wametoa ofa kwa Cengiz Under, wing'a mwenye miaka 21 wa Roma raia wa Uturuki. (Tuttomercatoweb, via Talksport)

Fulham huenda wakashindwa na Cardiff City kumsaini mshambuliaji wa Namtes raia wa Argentina Emiliano Sala, 28. (Mail on Sunday)Keylor Navas

Kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 32, hataondoka Real Madrid Mwezi Januari. (Marca)

Mshambuliaji wa Inter Milan raia wa Argentina Mauro Icardi, 25, anasema mazungumzo bado yanaendea na klabu kuhusu kuongezwa mkataba wake. (Goal)

Kocha wa PSV Eindhoven coach Mark van Bommel amezungumza na kiungo wa kati Arjen Robben kuhusu kurudi kwenye klabu. Robben ataondoka Bayern Munich mwisho wa msimu. (Bild - in German)
Bora kutoka Jumapili

Bournemouth na West Ham wanang'ang'ania kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na Ruben Loftus-Cheek, 22, huku vilabu hivyo viwili vikitafakari uwezekano wa kumchukua kiungo huyo kwa mkopo kabla ya kumpatia mkataba wa kudumu mwisho wa msimu huu. (Sun)

Chelsea wanapania kumsajili mshambuliaji wa England Callum Wilson anayechezea Bournemouth kwa kima cha euro milioni 30 mwezi Januari. (Express)

Lakini meneja wa Bournemouth, Eddie Howe anaamini klabu yake haitamuachilia nyota huyo wa miaka 26. (Goal)

Arsenal wamekubali kumchukua Denis Suarez, 24, kujaza pengo lililoachwa na Aaron Ramsey huku kiungo huyo wa kati wa Uhispania akitafuta njia ya kuihama Barcelona ili apate nafasi ya kucheza zaidi.

Ramsey anajiandaa kuhama Gunners kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu huu. (Independent)

Fulham wanataka kumsajili beki wa kati wa Gary Cahill, 32, kutoka kwa mahasimu wao Chelsea mwezi Januari. (Sky Sports)

Nahodha wa Manchester United Antonio Valencia, 33,yuko tayari kuhama klabu hiyo ifikapo mwezi Januari mwakani, baada ya kukubali kuwa hana uwezo wa kubadili matazamo wa meneja wake Jose Mourinho juu yake. (Mail)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post