MANARA AMVAA ZAHERA KUHUSU KAKOLANYA

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameibuka na kutoa maoni yake juu ya mlinda mlango wa Yanga, Beno Kakolanya ambaye amekataliwa na kocha wa klabu hiyo, Mwinyi Zahera.

Hayo yamekuja baada ya kocha wa Yanga kuonekana katika video moja akisema kuwa klabu hiyo haina haja ya kuendelea tena na Beno Kakolanya na badala yake atafute klabu nyingine inayoweza kumsajili, baada ya kugoma kucheza kutokana na kudai maslahi yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Haji Manara ameandika, "nahitaji povu la omo, la foma nimpelekee Congo Meneja huyu anayetajwa hakuwepo wakati Beno alipowaokoa na 'saves' zaidi ya kumi walipopaki basi miezi michache nyuma?. Jibu ni rahisi tu, wenzetu hubebana sana sana, hapo anatengenezewa mazingira 'papaa ndoki' aje kuwa nyanda namba one kama mnabisha muda utahukumu."Alisema Manara

Katika video maalum wakati akiongea na mtandao wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera alisema, "kurejea Yanga, hilo haliwezekani. Kesho (jana) dirisha litafungwa, sijui saa ngapi, wale waliomwambia asiende mazoezi, kama ni mameneja wake au ni watu gani, wao ndiyo wamtafutie timu ila hapa kwetu nadhani kama haiwezekani tena."

Dirisha la usajili limefungwa saa 6:00 usiku ya Disemba 15 na hatma ya Beno Kakolanya bado haijafahamika ni wapi ataelekea. Yanga inatarajia kushuka dimbani hii leo kukipiga na Ruvu Shooting, mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utaochezwa katika uwanja wa taifa.

Chanzo:Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post