MSEKWA ATOA NENO KWA MAGUFULI BAADA YA KUTEULIWA

Spika wa Bunge Mstaafu, Pius Msekwa amesema uteuzi wake wa kuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) uliofanywa na Rais John Magufuli Desemba 6 ,2018 haukuwa ni kwa makosa na kwamba Rais anatambua utendaji wake na uzoefu alionao kwa kuongoza baadhi ya vyuo vikuu nchini-kikiwapo Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

Msekwa amesema hayo wakati akizungumza katika mahafali ya sita ya chuo hicho, ambapo amesema kupitia nafasi hiyo atahakikisha chuo hicho kinakuwa chachu ya kuzalisha wataalamu wa nyanja mbalimbali na kwamba amekuwa na bahati ya kuteuliwa kwa awamu ya tatu sasa kuongoza vyuo vikuu nchini.

"Kwanza kuna kila sababu ya kumshukuru Rais kwa kuniona mimi nafaa kuvaa kiatu hiki kwani kuna watu wengi serikalini lakini kaona mimi ndiye sahihi zaidi, nitaitumia fursa hii kuboresha elimu ya sayansi na teknolojia sambamba na kuongeza udahili kwa mwaka 2019/2020", amesema Msekwa.

Naye mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, Zakia Meghji ameshauri uongozi wa chuo hicho kufanya tafiti katika nyanja mbalimba ili kuchochea maendeleo ya uchumi wa viwanda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post