PAPA FRANCIS ATOA UJUMBE WA KRISMASI,


Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, amewataka waumini wa kanisa hilo na wananchi wote duniani kuishi maisha ya kawaida yasiyokuwa na ujivuni wa mali bali yenye kumtukuza Mungu.

Papa ameyasema hayo katika Ibada ya Misa ya mkesha wa Krismasi ndani ya Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Vatican, misa ambayo ni mojawapo ya sherehe muhimu zaidi za Kikatoliki katika kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

''Kuzaliwa kwa Kristo kunamaanisha njia mpya ya kuishi nayo si kwa kuharibu na kutumia mali nyingi kwa kusherehekea lakini kwa kugawana na kutoa kwa kila mwenye uhitaji", amesema Papa Francis.

Papa pia amesisitiza kuwa ''chakula cha maisha sio utajiri wa mali lakini upendo, sio uovu lakini upendo, si uchafu lakini urahisi na hiki ndicho humpenda Mungu''.

Papa Francis leo mchana atatoa ujumbe wake wa sita wa Urbi et Orbi tangu alipochukua wadhifa huo. Mara nyingi ujumbe wa UrbI et Orbi hutumiwa kuomba amani ulimwenguni na hutolewa wakati wa Siku Kuu ya Pasaka, Krismasi na baada ya kuchaguliwa kwa Papa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post