BOHARI YA DAWA (MSD) YAPATA BODI MPYA YA WADHAMINI


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ` (kushoto), akimkabidhi vifaa vya kazi Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Udhamini ya Bohari ya Dawa (MSD), Dkt.Fatma Mrisho baada ya kuizindua rasmi Dar es Salaam 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo.
Mjumbe wa bodi hiyo, Dkt.Marina Njelekela, akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa bodi.
Baadhi ya maofisa wa MSD wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mjumbe wa bodi hiyo, Uphoo Swai akijitambulisha.
Mjumbe wa bodi hiyo, Bw.Ahmed Shaaban Kilima akijitambulisha.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu, akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu kuzindua bodi hiyo. 
Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dkt.Fatuma Mrisho, akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe ``wa bodi hiyo.
Na Dotto Mwaibale


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ` (Mb.) leo amezindua Bodi mpya ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) ambayo mwenyekiti wake ni Dr.Fatma Mrisho. 

Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ni pamoja na Bi. Uphoo Swai, Dkt. Eliamini Sedoyeke, Bw. Ahmed Shaaban Kilima, Bw. Mwemezi Elnathan Ngemera, Bw. Lubengo Hilary Nyang’ula, Prof. Eligius Francis Lyamuya na Dkt. Marina Daula Njelekela ``huku mjumbe mwingine wa Bodi hiyo akitegemewa kuteuliwa hivi karibuni.

Mhe. Ummy amewataka wajumbe wa bodi hiyo, kufanya kazi kama timu moja kwa kutumia taaluma na weledi wao ili kuhakikisha wanasimamia vyema utendaji wa shughuli za Bohari ya Dawa na kufikia viwango bora vya ufanisi zaidi katika ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.

Aidha amewasihi wajumbe hao kuhakikisha MSD inajiendesha kibiashara, sambamba na kuzingatia taratibu za kitaalamu zinazohusiana na usimamizi na udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na maelekezo ya sheria ya manunuzi ya umma.

Waziri Ummy ameielekeza bodi hiyo kuhakikisha Bohari ya Dawa inajiendesha vyema kifedha na shughuli zake kuendeshwa kwa gharama nafuu, kuziba mianya yote ya rushwa, wizi na ubadhirifu wa aina yoyote ile, upatikanaji wa Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi vyenye ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa na mwisho kusimamia, kuboresha na kudumisha matumizi ya tehama ili kuleta tija katika utekelezaji wa majukumu ya Bohari ya Dawa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527