WAZIRI MKUU AWATAKA MAWAZIRI KUTUMIA VIZURI MITANDAO YA KIJAMII

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka mawaziri na viongozi wengine wa Serikali kutumia vizuri mitandao ya kijamii ili kuepuka mambo ambayo jamii haikubaliani nayo.

Ametoa kauli hiyo jana Jumatatu Desemba 3, 2018 wakati akifungua mafunzo ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa jijini Dodoma.

“Jana nimewaambia mawaziri wote tuliojiunga katika mitandao hii tuitumie vizuri, wewe kama kiongozi wa Serikali unatakiwa kusoma kilichoandikwa kwenye mtandao na kuona umuhimu wa kwenda kuchangia ama la,” amesema Majaliwa.

Kwa upande wake ofisa mtendaji mkuu wa taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja amesema programu hiyo ya mafunzo ya uongozi, ni ya kwanza na ya aina yake iliyoandaliwa mahsusi kwa ajili ya viongozi hao.


“Lengo la programu hii ni kuimarisha uwezo wa wakuu wa mikoa na makatibu tawala katika kufanya uamuzi wa kimkakati, kuongoza watu na kusimamia rasilimali nyingine, pamoja na kujijengea sifa binafsi za uongozi,” amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527