CCM WAMTUHUMU MBATIA KUTAKATISHA FEDHA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi Vijijini kimeitaka serikali kuichunguza Taasisi ya Maendeleo Jimbo la Vunjo (VDF) kwa madai ya utakatishaji wa fedha.

Katika taarifa iliyosainiwa na Katibu wa CCM wilaya hiyo, Miriam Kaaya, chama hicho kimeitaka VDF ieleze ilianza na kiasi gani cha fedha na bajeti ya barabara inazozijenga ni kiasi gani.

“Tunaitaka VDF itamke wazi kuzithibitishia mamlaka za serikali ilianza na kiasi gani cha fedha katika akaunti yake na bajeti nzima ya mradi wa barabara za moramu kwa Jimbo la Vunjo,” imesema taarifa hiyo.

"Kwa kufanya hivyo itaondoa uwezekano mkubwa wa asasi hiyo kutumika katika vitendo vya utakatishaji fedha, hivyo tunaitaka serikali kusitisha shughuli za taasisi hiyo wakati uchunguzi ukiendelea. ” taarifa hiyo imesema.

Miongoni mwa viongozi wa bodi ya VDF ni Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia ambaye na mwenyekiti wake wamekanusha tuhuma hizo.

Mwenyekiti wa VDF ambaye ni Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Martin Shao amesema hawajapokea fedha yoyote kutoka nje na kwamba fedha wanazotumia kutekeleza miradi zinatoka kwa wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527