Picha : WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ZANAKI WATEMBELEA HIFADHI ASILI YA MAGAMBA LUSHOTO, TANGA

Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga Samiji Mlemba (katikati) akitoa maelezo kwa wanafunzi wa Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam waliopata ufadhili wa kutembelea hifadhi hiyo waliopewa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kupitia mradi wa Uwezo Award uliendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la Great Hope Foundation. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG - Lushoto.

Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga Samiji Mlemba akiwa ameongozana na kuwapa maelezo wanafunzi na wanahabari waliokuwa katika ziara hiyo.
Moja ya bango linalowakaribisha wageni katika hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga na kuwapa maelezo machache.
Wanafunzi wakiendelea na safari ambayo iliwachukua saa 3 kufika katika kilele kwa km 2.2.
Wanafunzi wakifurahia katika kituo cha kwanza ambacho kilikuwa ni Chanzo cha Maji.
Pichani ni wanahabari wa vyombo mbali mbali Msungu wa ITV (kwanza kulia) na Said Makala (wa pili toka kulia) wakifurahia pamoja na maofisa wa GHF Noela na Maria wa TTB... Juu ni Mwanahabari Cathbert Kajuna -Kajunason/MMG akiwa na wanafunzi wakifurahia katika kituo cha pili ambacho ni Mshai.
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga Samiji Mlemba akitoa maelezo machache wakati wanafunzi hao walipofika kituo cha Mshai wakielekea katika kilele cha mlima Kigulu Hakwewa.
Safari ya kuelekea katika kilele cha mlima wa Kigulu Hakwewa.
Safari ilikuwa ni ndefu ambapo wengine waliamua kupumzika ili kuweza kuvuta pumzi katika miti yenye umri wa miaka 40.
Muonekano wa miti mikubwa yenye kuvutia iliyoishi umri wa miaka 40 mpaka sasa.
Kila mmoja alikuwa na furaha kufika katika kituo cha tatu cha Kwesimu ambapo historia ya sehemu hiyo ilikuwa ni kupatikana kwa huduma za simu. Hapo ndipo mawasiliano ya simu yakipatikana yani namaanisha kila mtu mwenye simu alikuwa akifika hapo ili aweze kupata nawasiliamo (Network ilikuwa ikipatikana eneo hilo).
Eneo hilo la Kwesimu ndipo mkondo wa maji ulikuwa ukipita.
Wanafunzi wakifurahia katika mlango wa pango la Wajerumani walilolitumia katika vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea mwaka 1914 - 1918.
Wanafunzi wakifurahia na mwalimu wao walieambatana nae katika mlango wa pango la Wajerumani walilolitumia katika vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea mwaka 1914 - 1918.
Meneja Uhusiano wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) nae aliweza kupata wasaa katika lango la pango la Wajerumani lililotumika katika Vita vya kwanza vya Dunia 1914-1918.


Ndani ya pango la Wajerumani walilolitumia katika vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea mwaka 1914 - 1918.

Wanafunzi wakifurahia na Afisa Utalii, Samiji Mlemba (katikati) wakiwa kwenye geti la kuingia kilele cha mlima Kigulu Hakwewa.

 Kilele cha Mlima Kigulu Hakwewa ambapo ni (1840 A.M.S.L) Usawa wa Juu wa Kiwango cha Bahari.
Kila mmoja akifurahia...
Makulaji kidogo!
Kila mmoja akiwa na uso wa furaha baada ya kutoka kilele cha Mlima Mgulu Hakwewa.
Baada ya wanafunzi kutembelea kilele cha mlima Kigulu Hakwewa waliweza kufika katika Msitu wa Asili wa Mkusu unaolimilikiwa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ili kujionea maporomoko ya maji ya Mvueni.
Wanafunzi wakifurahia katika maporomoko ya maji ya Mvueni yaliyopo katika Msitu wa Asili wa Mkusu uliopo Lushoto, Tanga.
Maporomoko ya maji ya Mvueni yaliyopo katika Msitu wa Asili wa Mkusu uliopo Lushoto, Tanga.
Wanafunzi wakifurahia katika Maporomoko ya maji ya Mvueni.
---
Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga ni moja ya vivutio vya hifadhi 12 za mazingira asilia vinavyosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Watu wengi wamekuwa wakisahau kuwa utalii wa ikolojia nao unafaida kwa jamii yetu ili iweze kujifunza mambo mbali mbali kuhusu misitu na viumbe hai.

Wakizungumza kwa wakati tofauti mara baada ya kutembelea hifadhi ya mazingira ya Magamba, Mfaume Salehe Msasa amesema “Kuwa Coordinator wa ni bahati kwangu na furaha pia kwa kuwa nimejifunza vitu vingi sana tangia nimeaza kuvolunteer @greathopetz pia naendelea kujifunza kwamaana kuwa kujifunza hakunaga mwisho,"

Kwa kwaida kila mwaka @greathopetz hua tunatoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi pamoja na shule zinazofanya miradi bora zaidi. Mwaka huu tulikua na shule 100 ambazo zimefanya mradi na shule ambayo imefanya mradi bora zaidi nakuweza kuwa mshindi wa kwanza ni Shule ya Sekondari Zanaki. “Miradi ya mwaka huu imekua ni ya tofauti kubwa kwa mshindi wa mradi wa Uwezo Award kupata zawadi nyingi na wamepewa safari ya kitalii ya kwenda msitu wa Magamba kwa kudhaminiwa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Nae Meneja wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ameshukuru jinsi wanafunzi walikuwa na moyo wa kujifunza kuhusu mazingira na kuomba shule pamoja na wazazi waweze kujitokeza kuwapeleka watoto wao katika vivutio mbali mbali vya utalii wa ikolojia ambao watu wengi wamekuwa wakiusahau.

"Unajua watu wengi wamekuwa wakikimbiali kuangalia wanyama ila huku napo ni zaidi ya kule maana wale wanaopenda kuona mazingira yanavyotunzwa basi hawana budi kufika bila kukosa, tunawakaribisha watanzania wote hasa kipindi hiki cha likizo kwa wawalete watoto wao wajionee vivutio mbali mbali mbali," amesema Tulizo Kilaga

Great Hope Foundation - GHF ni shirika lisilo la kiserikali lililojikita katika kuwasaidia vijana kutambua na Kuendelea uwezo wao katika maeneo mbalimbali. Shirika hubuni na kuendesha miradi katika muktaadha wa kuwajengea uwezo Vijana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post