ALIKIBA AWEKA WAZI SABABU ZA KUINGIA UWANJANI NA USAFIRI BINAFSI, MECHI KATI YA MBEYA CITY NA COASTAL UNION


Msanii wa Bongofleva ambaye pia ni mwanasoka wa club ya Coastal Union ya TangaAlikiba, Jumapili ya December 9 2018 alipata nafasi kwa mara ya kwanza kuichezea timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Mkwakwani.

Alikiba alikuwa kivutia kikubwa katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya 1-1, lakini alisaidia pia upatikanaji wa goli la Coastal Union lilifungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 5 ya mchezo, baada ya Alikiba kusababisha kona iliyozaa goli hilo, game hiyo Alikibaalicheza kwa dakika 64 tu na kufanyiwa na mabiliko na kocha Juma Mgunda.

Kingine kilichoshangaza wengi ni kuwa Alikiba aliingia uwanjani hapo akiwa na gari lake binafsi na sio usafiri wa timu kama walivyoingia wachezaji wenzake, akihojiwa Azam TVbaada ya mechi Alikiba kataja sababu 

“Ni mara ya kwanza kwangu kwa hivyo ni chalenji nilikuwa nimeipata kwa ajili ya hofu, natamani hata hii leo ningefunga lakini mpira hautabiriki, mimi sikai kambini nakaa kwenye nyumba yangu huku kwa hiyo huwa tunakutana hapa”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post