JWTZ YATANGAZA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI MADAKTARI WA BINADAMU,FANI ZA TIBA

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini Madaktari wa Binadamu na fani nyingine za Tiba.

Nafasi hizo zinatolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa huduma za afya katika Hospitali zetu, vituo vya afya na Zahanati kulingana na mahitaji  ya sasa na siku zijazo.

Watakao andikishwa Jeshini ni wale wenye taaluma zifatazo:-

a. Daktari Bingwa wa Meno    -  Dental Surgeon

b. Daktari Bingwa     -       Specialist Neurasurgeon

c. Mkemia   (Chemisist)

d.Mteknolojia Msaidizi (Maabara) - Assistant Laboratory Technician.

e. Tabibu msaidizi     -  Assistant Clinical officer.

f. Katibu wa Hospitali  -

g.Msaidizi wa kumbukumbu.  – Medical Records (Certificate)

h. Daktari  - Medical Doctors.

j. Afisa Muuguzi  -  Registered Nursing Officer.

k. Fundi sanifu vifaa tiba  -  Bio Medical Engineer.

l.  Tabibu   - Clinical Assistant  (Certificate).

m. Mteknolojia msaidizi -  Laboratory Assistant (Certificate)

n. Mfamasia -  Pharmacist  (Degree)

o. Mtoa tiba kwa vitendo  - Physiotherapist  (Diploma)

p.  Afisa Muuguzi msaidizi  - Assistant Nursing officer

Sifa za kuandikishwa Jeshini ni zifuatazo:-

a.  Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

b. Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 28 isipokuwa specialist

c. Awe na afya njema ya mwili na akili timamu.

d.  Awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri

e. Awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai Mahakamani na kufungwa jela.

f. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate), vyeti vya shule (Academic & School Leaving Certificates) na vyeti vya Chuo (Transcript & Academic Certificates).

g. Kama ni Daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo (Internship) na kutunukiwa vyeti pamoja na kusajiliwa na Bodi.

h.Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo.

Wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania waripoti katika Kambi yaJenerali Abdallah Twalipo, Mgulani    Dar es Salaam tarehe              17, Desemba, 2018 kuanzia saa 1.00 Asubuhi kwa usaili.

Waombaji wafike na vyeti halisi (Original Certificates) vya kuzaliwa na masomo pia wajitegemee kwa usafiri, chakula na malazi.

Aidha, watakaochaguliwa na kuandikishwa Jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali ya Jeshi na yatakayo waendeleza katika taaluma zao. Wakiwa Jeshini majukumu watakayopatiwa ni yale yatakayowapa changamoto na fursa nzuri za kutumia taaluma zao.

JIUNGE NA JWTZ UJIFUNZE MENGI, UONE MENGI NA UFAIDI MENGI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post