KAULI YA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KUANGUKA JUKWAANI SUMBAWANGA.... "HAKIKA MCHEZO USIUCHEZEE..MMENISHINDA TABIA"

Siku moja baada kudondoka jukwaani kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mwanamuziki Diamond platnumz amewavulia kofia wakazi wa mkoa huo.

Diamond kupitia akaunti yake ya Instagram aliandika; Hakika mchezo usiuchezee… Sumbawanga mmenishinda tabia jamani. Rayvanny, Mbosso Zanzibar! Zanzibar! tukutane Uwanja wa Amani siku ya Jumanne Desemba 11.’

Tukio la kuanguka jukwaani kwa Diamond lilitokea jana kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, wakati akiimba wimbo wa ‘Zilipendwa’ akiwa na wasanii Rayvanny na Mbosso.


Diamond aliyekuwa kifua wazi huku akiwa amevaa suruali yenye ufito mweupe pembeni, ubao uliokuwa umewekwa chini ulisogea na kujikuta anaanguka kwa kudumbukia chini ya jukwaa hilo, jambo lililozua gumzo mitandaoni.


Akizungumzia tukio hilo, Meneja wa Diamond, Babu Tale alikiri kuwa kilichoonekana kwenye video mtandaoni ndicho kilichotokea.


Tale amesema moja ya sababu ya msanii wake huyo kudondoka ni kutokana na kucheza kwa kurukaruka kwa nguvu jukwaani.


Msikilize Diamond hapo chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527