DISCO TOTO YAPIGWA MARUFUKU DAR

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hatarajii kuona 'disco-toto' ikifanyika popote pale jijini Dar katika kuadhimisha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Ameeleza kuwa hadi sasa hakuna aliyepeleka maombi kwa jeshi hilo ili kutoa huduma hiyo kwenye siku za sikukuu, ili ukaguzi wa kina ufanyike kwenye kumbi hizo kwa ajili ya usalama wa watoto.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Desemba 22, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Mambosasa ametoa kauli hiyo wakati akieleza jinsi polisi walivyojipanga kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.


Amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao katika kusherehekea sikukuu hizi ili kuepusha matukio ya watoto kupata ajali, kupotea na kuzama kwenye fukwe, kama ilivyokuwa ikitokea miaka ya nyuma.

“Wazazi katika kipindi hiki cha sikukuu kila mmoja atimize wajibu wake wa kuhakikisha anajilinda yeye mwenye na watoto wake kwa kufanya hivyo sikukuu hii haitakuwa na madhara kwao.

“Ngoma za vigodoro haziendani na ustaarabu wa Dar es Salaam na niseme tu kwamba tutakushugulikia kabla hata haujaanza kucheza ngoma hiyo”.


Kamanda Mambosasa pia ametoa wito pia kwa wakazi wa Dar es Salaam kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote katika maadhimisho ya sikukuu hizo ili kuwepo na amani na usalama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527