Tuesday, December 4, 2018

CHID BENZ ADHAMIRIA KUWA SHEIKH..MUNGU NISAIDIE NINA UCHAFU

  Malaki Philipo       Tuesday, December 4, 2018
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mkali wa michano , Rashid Makwilo maarufu kama Chid Benz, amefunguka mipango yake ya kuachana na muziki na kumtumikia Mungu.

Chid benz amesema kwamba kitendo cha kukutana na Sheikh Abdulrazac ni kama moja ya njia ya kufikia malengo yake, kwani anamsaidia kumkuza kiroho.

“Muziki ni kitu hatari sana, kama hivi unaona niko na sheikh maana yake kuacha maisha hayo ya muziki na stori za muziki tunahitaji watu kama hawa, ili watufundishe mambo hayo ya huku, katika maisha sisi vijana tunavyoishi tunasafiri kule na huku, mimi naweza muziki sana, yeye anaweza kurutubisha maombi yako na yake yaungane kuyasogeza kwa mwenyezi Mungu, ni yeye anisaidie mimi kwa njia gani niweze kufikisha maombi yangu kwa mwenyezi Mungu, inawezekana naomba kila siku lakini hunisikii kutokana nina uchafu labda”, amesema Chid Benz

Ikumbukwe kwamba sheikh huyo hivi karibuni aliweka wazi mipango yake ya kumbadilisha Chid Benz ili aache muziki na kumtumikia Mungu, hususan kwenye kipindi ambacho Chid anaonekana kuanza kusimama badala ya kupitia misukosuko mingi kwenye maisha ya sanaa na ujana.

Iwapo Chid Benz atafikia hatua hiyo, ataungana na Mzee Yusuph, Suma Lee na Saigon, ambao waliamua kuacha bongo fleva na kuwa waumini wazuri wa dini huku wakimtumikia Mungu.

Chanzo:Eatv
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post