BOSI WA CIA KUHOJIWA MAUAJI YA KHASHOGGI

Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani Bi Gina Haspel atafanya mahojiano na wajumbe wa bunge la Congress juu ya mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi.

Vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti kuwa bi Haspel atakutana na viongozi wa bunge la Seneti baadae leo Jumanne.

Mkurugenzi huyo hakuwepo wiki iliyopita wakati mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi walipofanya mazungumzo na viongozi wa Seneti, kitendo ambacho kiliwakasirisha baadhi ya wajumbe wa bunge hilo.

Khashoggi aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2. Mwanahabari huyo alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa sera za Saudia hususani mwanamfalme Mohammed bin Salman.

Vyombo vya habari vya Marekani pia vimeripoti kuwa ripoti ya CIA juu ya mkasa huo inaonesha kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa bin Salman aliamuru mauaji hayo.

Tayari Saudia imewashitaki watu 11 juu ya mauaji hayo, lakini wanakanusha vikali juu ya uhusika wa bin Salman.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527