ASKARI MAGEREZA AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI


Askari Magereza katika Gereza la Kilimo Kitai wilayani Mbinga, Ruvuma, Adamu Kulwa Mgaga (24), amejiua kwa kujipiga risasi.

Askari hiyo mwenye namba B:8400 WDR, amejiua akiwa lindo la mifigo kwa kujipiga risasi eneo la kidevu na kusababisha kichwa kupasuka

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Ruvuma, Arekizanda Nyifwa, alithibitisha kutokea kwa tuko hilo Desemba 25, mwaka huu, saa 2:30 usiku katika gereza la Kitai-Mbinga.

Alisema askari huyo alipokuwa lindo ilipofika saa 2:30 usiku alichukua bunduki aliyokuwanayo aina ya SAR na kuelekeza bomba kwenye kidevu chake kisha kuhesabu moja hadi tatu na kufyatu risasi ambazo zilifumua kichwa chake na kufariki dunia papo hapo. 


Alisema askari huyo alifanya hivyo akiwa katika sare za jeshi hilo na kwamba chanzo cha kujiua bado hakijafahamika kwa kuwa hakuacha ujumbe wowote.Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post