Picha 10 Gumzo : MREMBO AMWENDESHA MME WAKE KWENYE TINGA TINGA WAKIFUNGA NDOA


Mrembo Lilian Peter Ndagiwe mkazi wa Shinyanga Mjini amezua gumzo wakati akifunga ndoa na Ottoh Yanga baada ya kupanda na kuendesha Mtambo 'Tinga Tinga' /Caterpillar ambalo hulitumia katika kazi zake katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.



Wanandoa hao wamepanda kwenye Mtambo huo muda mfupi leo Disemba 28,2018 walipomaliza kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Buhangija mjini Shinyanga.



Kama ilivyozoeleka kuwa wanandoa hupanda kwenye magari, lakini kwa wanandoa hawa hali imekuwa tofauti kabisa kwani wao wameamua kupanda kwenye tinga tinga la kutengenezea barabara na kupita nalo mtaani. 



Imeelezwa kuwa bibi harusi Lilian Peter ni mtaalamu wa kuendesha Mtambo huo, kutokana na mahaba aliyonayo kwenye kazi yake ,ili kukamilisha furaha yake ya ndoa basi kaamua kuendesha Tinga Tinga na hakuona haja ya kupanda kwenye gari na mmewe.


Mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametusogezea picha hapa chini

Bibi Harusi Lilian Peter Ndagiwe akijiandaa kupanda kwenye tinga tinga

Bibi Harusi Lilian Peter Ndagiwe akipanda kwenye tinga tingaBibi Harusi Lilian Peter Ndagiwe akiwa wenye tingatinga

Bibi Harusi Lilian Peter Ndagiwe  na bwana harusi Otto Yanga wakiwa kwenye tingatinga
Bibi Harusi Lilian Peter Ndagiwe akiendesha tingatinga
Wakipita mtaani na tingatinga lao

Msafara wa harusi

Kikazi zaidi : Lilian Peter Ndagiwe akiwa kwenye mtambo kabla ya kufunga ndoa 

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post