TCAA YAWAJENGEA UWEZO WANAHABARI KUHUSU MASUALA YA USAFIRI WA ANGA


Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), Aristid Kanje akizungumza na wanahabri waliohudhuria katika mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzana (TCAA) ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Anga Duniani ambapo kilele chake ni Desemba 7, 2018. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wanahabari waliohudhuria semina ya kuwajengea uwezo kuhusu Usafiri wa Anga iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakifuatilia kwa karibu semina hiyo.
 ****


Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzana (TCAA) imefanya semina ya kuwajengea uwezo wanahabari jijini Dar es Salaam ili kujua masuala ya usafiri wa anga.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), Aristid Kanje amewashukuru wanahabari wa kutenga muda wao na kuhudhuria mafunzo hayo ili kuweza kuwajengea uwezo katika uandishi.

"Jambo lililonifurahisha ni jinsi mlivyoweza kujitoa na kuhudhuria mafunzo ili kuweza kuongeza uwezo na ujuzi katika uandishi wenu juu ya masuala ya ya anga," amesema Bw. Kanje.

Mmoja ya washiriki wa semina hiyo, Moses Mohamed amewashukuru mamlaka kwa kuweza kuona umuhimu wa kuwapa mafunzo yaliyoongezea weledi wa kutambua masuala mazima ya usafiri wa anga.

"Nitoe shukrani zangu za pekee kwa TCAA kwa hili walilofanya japo unaweza kuliona dogo ila limeongeza kitu kikubwa katika uandishi wangu," amesema Moses.

Semina hiyo ni muendelezo ya matukio ambayo hufanyika katika maadhimisho ya maadhimisho ya wiki ya Anga Duniani ambapo kilele chake ni Desemba 7, 2018.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post