Saturday, November 10, 2018

Breaking News : WAZIRI MWIJAGE NA TIZEBA WATUMBULIWA...RAIS MAGUFULI ASUKUMIA NDANI WENGINE

  Malunde       Saturday, November 10, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, leo Novemba 10, 2018, ametengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba.

Taarifa iliyotumwa na Mkurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa, imeeleza nafasi ya Dkt Charles Tizeba imeshikwa na Japhet Hasunga, ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

Aidha katika nafasi ya viwanda na biashara iliyokuwa chini ya Charles Mwijage, imechukuliwa na Joseph Kakunda, ambaye naye kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa TAMISEMI.

Aidha Rais Magufuli amemteua Constantine John Kanyasu kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, pamoja na kumteua Profesa Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala bora.

Aidha Rais Magufuli, amemteua Innocent Lugha kuwa naibu Waziri wa Kilimo, na uteuzi wa viongozi unaanz a Novemba 10, na wataapishwa Jumatatu Ikulu Jijini Dar es salaam.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post