WAZALISHA MVINYO WA MATUNDA NCHINI WAIOMBA SERIKALI KUWAPUNGUZIA KODI YA USHURU WA BIDHAA


Chama cha wazalishaji wa mvinyo wa matunda Tanzania (TALMA) kimeiomba Serikali kupunguza kodi ya ushuru wa bidhaa kutoka shilingi 200 hadi 63 kwa lita moja, hatua
itakayosaidia wazalishaji wa bidhaa hiyo kumudu gharama za uendeshaji.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Adolf Olomi kwenye mkutano wa kifaifa uliofanyika jana Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na taasisi mbalimbali za Serikali
ikiwemo mamlaka ya mapato nchini TRA, shirika la viwango Tanzania TBS pamoja na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO.

Aidha Olomi alitoa rai kwa wazalishaji wa mvinyo nchini kuhakikisha wanasajili bidhaa zao ili kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ambapo kupitia mkutano huo taasisi na
mamlaka mbalimbali za serikali zilitoa semina namna ya kutekeleza suala hilo.

Nao baadhi ya wazalishaji wa mvinyo, Straton Mzee kutoka kampuni ya Yande Investment ya Jijini Mwanza inayozalisha mvinyo wa “Harambee Banana Wine” pamoja na Anna
Barnabas kutoka kampuni ya Bhunu Mbundi ya Jijini Arusha, wamesema kiwango kikubwa cha kodi ushuru wa bidhaa inahatarisha ukuaji wa wazalishaji wengi wa
mvinyo nchini na hivyo kukwamisha kufikiwa kwa Tanzania ya Viwanda.

Mkuu wa Idara ya Huduma na Elimu (TRA) Mkoa Mwanza, Lutufyo Mtafya alisema ikiwa wazalishaji hao wanaona utekelezaji wa kodi ya ushuru wa bidhaa unakuwa mgumu
kutokana na ukubwa wa gharama, wanaweza kuwasilisha serikalini mapendekezo yao kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho kwa mujibu wa sheria.

Na George Binagi-GB Pazzo
Mwenyekiti wa chama cha wazalisha mvinyo kwa kutumia matunda (TALMA), Adolf Olomi akizungumza wenye mkutano wa chama hicho uliofanyika Jijini Mwanza.
Washiriki wa mkutano huo
Tazama Video hapa chiniDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527