Picha : UMOJA WA WAKE WA VIONGOZI TANZANIA WACHANGIA MILIONI 100 KUJENGA MADARASA NA VYOO BUHANGIJA -SHINYANGA

Umoja wa Wake wa Viongozi waliopo madarakani sasa na waliokuwepo zamani nchini Tanzania 'New Millennium Women Group - NMWG' umechangia shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne na matundu nane ya vyoo kwa katika shule ya msingi Buhangija mjini Shinyanga inayolea watoto wenye ualbino,wasioona na wasiosikia.

Akizungumza leo Jumanne Novemba 13,2018 alipotembelea shule hiyo,Mlezi Mstaafu wa Umoja huo,Tunu Pinda alisema fedha hizo ni sehemu ya michango ya wanachama wa umoja huo na Harambee kuchangia kituo cha Buhangija iliyofanyika Desemba 12,2014 jijini Dar es salaam.

Tunu Pinda aliyekuwa ameambatana na Mama Matrida Balama,Mama Germina Lukuvi,Mama Naima Malima, Msanii Keisha na Mkuu wa wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi alisema fedha hizo zitatumika kujenga madarasa manne na matundu 8 ya vyoo katika shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 1058 kati yao wenye ualbino ni 131.

“Umoja huu ambao sasa mlezi wake ni Mke wa Waziri Mkuu,Mama Mary Majaliwa tulitembelea kituo hiki,kama wazazi tuliguswa changamoto zinazowakabili ndugu zetu wenye ualbino vikiwemo vitendo vya mauaji ya watu wenye ualbino”,alisema.

“Kutokana na changamoto hizo,wake wa viongozi waliopo madarakani na waliostaafu tuliamua kuiunga mkono serikali kuwalinda watu wenye ualbino kwa kufanya harambee kwa ajili ya vijana na watoto wetu waliopo Buhangija”,aliongeza.

Tunu aliiomba serikali ya mkoa wa Shinyanga kusimamia ujenzi wa madarasa na matundu hayo ya vyoo ili pesa zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kuepuka vitendo vya uchakachuaji.

Kwa upande wake Msanii Khadija Shaban Ntaya maarufu Keisha alisema pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo watu wenye ualbino ambazo ni pamoja na saratani ya ngozi na macho ni vyema watoto wenye ualbino kusoma kwa bidii na kutokata tamaa ili kufikia malengo yao.

Naye Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela aliwashukuru wake hao wa viongozi kwa msaada huo na kuahidi kutumia fedha hizo vizuri na kwamba ujenzi utaanza mara moja akieleza kuwa hadi kufikia Machi 1,2019 ujenzi utakuwa umekamilika.

Wakiwa katika kituo cha Buhangija,Tunu Pinda na wenzake walitembelea eneo ambapo ujenzi wa madarasa na vyoo utafanyika huku wakikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto ambazo ni pamoja na taulo laini kwa wasichana,juisi,maziwa,biskuti,kalamu,penseli na madaftari.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyang, Jasinta Mboneko akimpokea Mlezi Mstaafu wa Umoja wa Wake wa Viongozi waliopo madarakani sasa na waliokuwepo zamani nchini Tanzania ‘New Millennium Women Group (NMWG)’,Tunu Pinda alipotembelea kituo cha Buhangija kilichopo katika manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Novemba 13,2018 – Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Mlezi Mstaafu wa Umoja wa Wake wa Viongozi waliopo madarakani sasa na waliokuwepo zamani nchini Tanzania ‘New Millennium Women Group (NMWG)’,Tunu Pinda akisalimiana na watoto wenye ualbino,wasiosikia na wasioona wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Mama Tunu Pinda,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko na viongozi mbalimbali wakisalimiana na watoto katika kituo cha Buhangija.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija.
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akiwakaribisha Wanachama wa Umoja wa Wake wa Viongozi waliopo madarakani sasa na waliokuwepo zamani nchini Tanzania ‘New Millennium Women Group (NMWG)’ wakiongozwa na Tunu Pinda waliotembelea kituo cha Buhangija leo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza wakati akiwakaribisha wanachama wa Umoja wa Wake wa Viongozi waliopo madarakani sasa na waliokuwepo zamani nchini Tanzania ‘New Millennium Women Group (NMWG).
Mlezi Mstaafu wa Umoja wa Wake wa Viongozi waliopo madarakani sasa na waliokuwepo zamani nchini Tanzania ‘New Millennium Women Group (NMWG)’,Tunu Pinda akizungumza katika kituo cha Buhangija na kuwaomba viongozi wa serikali ya mkoa wa Shinyanga kusimamia ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule ya msingi Buhangija ili shilingi milioni 100 walizotoa ziwe na tija.
Tunu Pinda ambaye ni mke wa Waziri Mkuu Msaafu Mizengo Pinda akizungumza katika kituo cha Buhangija.
Watoto wakimsikiliza Mama Tunu Pinda.
Mlezi Mstaafu wa Umoja wa Wake wa Viongozi waliopo madarakani sasa na waliokuwepo zamani nchini Tanzania ‘New Millennium Women Group (NMWG)’,Tunu Pinda akiimba wimbo na watoto wa kituo cha Buhangija.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akiwashukuru wake wa viongozi nchini kwa kujitoa kusaidia watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija na kuahidi kusimamia fedha zilizotolewa na New Millennium Women Group.
Mkuu wa wilaya ya Butiama mkoani Mara,Annarose Nyamubi aliyekuwa ameambatana wanachama wa New Millennium Women Group akizungumza katika kituo cha Buhangija. Nyamubi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakati harambee iliyoendeshwa na wake wa viongozi mwaka 2014 kwa ajili ya kusaidia watoto na vijana wa kituo cha Buhangija na kufanikisha kupatikana kwa shilingi milioni 100 ambazo zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Buhangija.
Mkuu wa wilaya ya Butiama mkoani Mara,Annarose Nyamubi akiwashukuru wadau mbalimbali wanaoendelea kuwasaidia watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija.
Mkuu wa shule ya msingi Buhangija,Selemani Kipanya akitoa taarifa kuhusu mafanikio na changamoto zilizopo katika shule/kituo cha Buhangija.Alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madarasa na matundu ya vyoo.
Wa kwanza kushoto ni Katibu wa New Millennium Women Group (NMWG),Naima Malima akifuatiwa na Msanii Khadija Shaban Ntaya maarufu Keisha na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko wakiteta jambo katika kituo cha Buhangija.
Mwanachama wa New Millennium Women Group, Mama Matilda Balama akizungumza katika kituo cha Buhangija.
Mwanachama wa New Millennium Women Group,Mama Germina Lukuvi akizungumza katika kituo cha Buhangija.
Msanii Khadija Shaban Ntaya maarufu Keisha akielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ualbino ambazo ni pamoja na saratani ya ngozi na kutoona vizuri hali inayosababisha wakati mwingine kukata tamaa katika maisha.
Msanii Keisha akiwashauri watoto wenye ulemavu kusoma kwa bidii na kuepuka kukata tamaa ili watimize ndoto zao.
Katibu wa Umoja wa Wake wa Viongozi waliopo madarakani sasa na waliokuwepo zamani nchini Tanzania maarufu New Millennium Women Group (NMWG),Naima Malima akizungumza wakati wanachama wa NMWG wakikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto waliopo kwenye kituo cha Buhangija ambazo ni pamoja nataulo laini kwa wasichana,juisi,maziwa,biskuti,kalamu,penseli na madaftari. 
Katibu wa NMWG ,Naima Malima akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo zilizomo kwenye maboksi hapo chini.
Wake wa Viongozi waliopo madarakani sasa na waliokuwepo zamani nchini Tanzania maarufu New Millennium Women Group wakigawa zawadi ya biskuti watoto hao.
Mtoto akipokea zawadi ya juisi kutoka kwa msanii Keisha.
Zoezi la kugawa zawadi kwa watoto likiendelea.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga,Magedi Magezi akigawa zawadi ya penseli kwa watoto.
Zoezi la kugawa zawadi likiendelea..
Wanachama wa New Millennium Women Group wakigawa taulo laini 'Pedi' kwa wasichana wanaolelewa katika kituo cha Buhangija.
Zoezi la kugawa taulo laini likiendelea.
Ugawaji pedi 'taulo laini ukiendelea'..
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buhangija,Selemani Kipanya akiwaonesha Wanachama wa Umoja wa Wake wa Viongozi waliopo madarakani sasa na waliokuwepo zamani nchini Tanzania maarufu New Millennium Women Group (NMWG) eneo ambapo patajengwa madarasa.
Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akionesha eneo ambapo patajengwa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Buhangija.
Wanachama wa Umoja wa Wake wa Viongozi waliopo madarakani sasa na waliokuwepo zamani nchini Tanzania 'New Millennium Women Group' na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527