MSULI WA MAGUFULI KWENYE KOROSHO WAMKUNA KHERI JAMES ...SHINYANGA WATAKA AGEUKIE MAZAO MENGINE

Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)taifa umempongeza Rais wa Tanzania John Magufuli kutatua sintofahamu kwa wakulima na soko la korosho nchini na kuwataka viongozi mbalimbali kuiga mfano wa uthubutu kwenye masuala ya kimaendeleo. 

Akizungumza leo Jumanne Novemba 13,2018 kwenye kikao kazi na madiwani wa halmashauri za mkoa wa shinyanga,Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Kheri James amesema viongozi wa chama na wale wa serikali  wanapaswa kuiga mifano kadhaa ya utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii zinazofanywa na rais Magufuli. 

Aliongeza kuwa viongozi wameshindwa kuiga nyendo za Rais Magufuli kutatua kero katika maeneo yao hali inayosababisha migogoro kati ya wananchi na serikali. 

“Uthubutu ambao ameuonyesha rais Magufuli ni ishara kwa viongozi wa chama na serikali kuiga mfano wake namna anavyopambana kuwainua watu wa hali ya chini ambao wanahitaji msaada hasa wakulima wanaotegemea kilimo kuendesha maisha yao”, alisema James.

“Nitumie fursa hiii nikiwa hapa mkoani Shinyanga,kuipongeza dhamira ya kweli naya haki,tunampongeza sana kwa uamuzi alioufanya na tunawaomba wakulima wa korosho watembee kifua mbele,kwani huu ni mwanzo wa muendelezo wa maslahi mapana ya taifa",alisema.

"Pamoja na pongezi hizi tunawatakia kila lakheri wateule walioteuliwa kwenda kubeba dhamana ya kilimo na biashara,waende kumsaidia rais katika maono yake ya kumuinua mkulima wa chini,ni imani yangu mawaziri hawa watakuwa ni kichocheo katika muendelezo wa kazi zinazofanywa na mheshimiwa rais”,aliongeza James.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa alisema hatua mbalimbali zinazochukuliwa dhidi ya maendeleo ni ilani ya chama hicho na kwamba zinasaidia kuleta maendeleo kwa wananchi na ndani ya chama. 

“Hatua zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya rais magufuli ni ilani ya Chama cha Mapinduzi na inaleta unafuu kwa wakulima na wananchi wa kipato cha chini”,alisema. 

Kwa upande wa wajumbe wa kikao kazi hicho madiwani kutoka halmashauri za mkoa wa shinyanga pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi ambapo diwani wa kata ya kambarage Hassan Mwendapole na Boniface Butondo wa kata ya Lagana wamepongeza hatua ya Rais Magufuli kulisimamia zao na soko la korosho na kuiomba serikali kuweka nguvu hiyo kwenye mazo mengine ya kibiashara likiwemo zao la pamba,kahawa na tumbaku.

Tazama picha za matukio hapa chini  
Mwenyekiti UVCCM Kheri James akizungumza kwenye kikao kazi chake na madiwani wa mkoa wa Shinyanga.Picha zote na Malaki Philipo.
Wajumbe wa kikao kazi wakiwa kwenye kikao.
Madiwani wa halmashauri za mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza katika kikao hicho.
Kikao kinaendelea
Wajumbe wa kikao wakisikiliza kwa umakini kinachoendelea ukumbini.
Wajumbe wakichangia maoni mbalimbali kwenye kikao.

Picha zote na  Malaki Philipo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post