SERIKALI KUWAPANDISHA VYEO ASKARI WALIONUSURIKA KIFO


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Kangi Lugola amemhakikishia Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza Jonathani Shanna kuwa atawapandisha vyeo askari waliofanikisha kuua majambazi Novemba 16.

Akiongea 
 jijini Mwanza ambapo yupo kwenye ziara ya kikazi, Kangi amesema anatambua kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi mkoani humo huku akiweka bayana kuwa askari waliojeruhiwa kwenye mapambano na majambazi wameonesha ushujaa kwani ni kosa kwa askari kuwa mwoga.

"Kwenye sheria yetu ya Jeshi la polisi na polisi wasaidizi sura ya 322, ukienda kwenye makosa ya kinidhamu ya askari, ni kosa kwa askari kuwa mwoga,''askari hupaswi kukimbia tukio' lazima ukabiliane nalo'', amesema.

''Nikuhakikishie Kamanda Shanna wale vijana wote waliofanya kazi kubwa kwenye tukio la juzi kukabiliana na majambazi, mimi kama Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi kwa amri ya Serikali tutawapa zawadi ya kuwapandisha vyeo", aliongeza Kangi Lugola.

Jumla ya watu saba wanaodaiwa kuwa majambazi waliuawa katika mapambano ya kujibizana kwa risasi na askari polisi katika tukio lililotokea alfajiri ya Novemba 16 katika eneo la mlima Kishiri jijini Mwanza.

Chanzo :- Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post