USHINDI WA MAN U WAMCHANGANYA MOURINHO,APIGA CHUPA ZA MAJI CHINI .

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ameeleza sababu iliyompelekea kupiga chupa za maji chini baada ya timu hiyo kufunga bao dakika za mwisho dhidi ya Young Boys kwenye mchezo huo wa Champions hatua ya mtoano uliyomalizika kwa bao 1 – 0.

Kwa mujibu wa Fox Sports alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, Mreno huyo amesema kuwa kitendo kile haikuwa hasira bali ilikuwa ni kuchanganyikiwa baada ya kupatikana kwa bao.

“Ni kuchanganyikiwa kabla ya hapo na baada ya kupatikana kwa bao. Nafikiri hatukuwa tunacheza ili kutoka sare, hatukuwa tunacheza hivyo ili kuwa katika matatizo hadi dakika za mwisho kwa hiyo ni kuchanganyikiwa,” amesema Mourinho.

Baada ya kutoa sababu hizo za kupiga chupa chini baada ya kupatikana kwa bao hilo ndipo, Mourinho akaamua kuwakumbusha wakosoaji wake kwa kuanika rekodi zake katika michuano hiyo Ulaya.

“Wacha ni tume ujumbe kwa wapenzi wangu na kuwaambia kwamba nimecheza michuano ya Champions League kwa miaka 14 na kufuzu hatua hii mara 14 .”

“Na katika miaka miwili ambayo sikushiriki Champions League, nilitwaa taji la Europa League mara mbili, kwa hiyo kwa miaka 16 mara 14 nimefuzu na mara mbili nisizoshiriki nimecheza Europa League na kutwaa taji.” alimalizia hivyo Mourinho.

Akizungumzia ushindi huo wa 1 – 0, Marouane Fellaini ambaye ndiye aliyefunga bao hilo amesema kuwa ilikuwa ni muda muafaka kwa yeye kuipatia bao hilo timu yake ya Man United huku akiwaeka sawa wale wanaoamini kuwa kabla ya kufunga goli hilo mpira alikuwa ameushika na kudai kuwa kwake anaamini mkono wake hakuupeleka katika mpira bali mpira uliufuata mkono.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post