KANGI LUGOLA NA UMMY KUSHIRIKI MAZISHI YA WATU 15 MKOANI MARA

Mawaziri wawili wanatarajiwa kushiriki mazishi ya watu 15 kati ya 16 waliofariki kwenye ajali iliyohusisha magari mawili ya abiria katika kijiji cha Komaswa wilayani Tarime mkoa wa Mara Jumatatu iliyopita.


Mawaziri hao ni waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu ambaye tayari amefika mkoani Mara na Kangi Lugola wa mambo ya ndani ambaye anatarajiwa kuwasili wakati wowote kuanzia sasa.

Watu hao walifariki baada ya magari madogo ya abiria ‘Hiace’ yanayofanya safari zake kati ya Musoma -Tarime na Tarime- Busurwa wilayani Rorya ambayo yaligongana uso kwa uso na kisha kulipuka moto.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amesema tayari maandalizi yamekwisha fanyika ikiwa ni pamoja na kuchimbwa makaburi na majeneza kwa ajili ha mazishi.

Wengine wanaotarajiwa kushiriki ni wakuu wa wilaya za mkoa wa Mara pamoja na viongozi mbalimbali wa kisiasa.

Katika ajali hiyo watu 15 walifariki papo hapo huku wengine wanne wakinusurika ingawa mmoja alifariki njiani wakati wakipelekwa hospitalini.

Chanzo:Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527