TEKNO AKUMBWA NA GONJWA HATARI,SASA KUKAA NJE YA MUZIKI


Uongozi wa msanii wa muziki nchini Nigeria, Tekno Miles, umewataka mashabiki kumuombea msanii huyo kutokana na ugonjwa unaomsumbua, ambao utamuhitaji kukaa nje ya muziki kwa muda.

Kwenye ukurasa wa instagram wa Mr. Ubi Franklin ambaye ni CEO wa kampuni inayomsimamia Tekno, umewekwa post inayotoa taarifa rasmi juu ya hali ya msanii huyo, na kuutaarifu umma kuwa kwa sasa hatofanya kazi za muziki ili kupata matibabu zaidi na kujipa muda wa kupona.

'Post' hiyo imesema kwamba kwa muda wa miezi miwili ilikuwa migumu kwa msanii Tekno kutokana na ugonjwa uliokuwa ukimsumbua ambao mwenyewe aliamini utaisha baada ya muda, lakini kutokana na hali yake kuwa si nzuri madaktari wameshauri asifanye kazi za muziki, ili aweze kupona zaidi.

Uongozi huo ulienda mbali zaidi kwa kusema kuwa Tekno amepata hitilafu kwenye mfumo wake wa saut kutokana na kuchoka kwa kazi nyingi na kuperform mara kwa mara, lakini atakuwa sawa na kazi zitaendelea kama kawaida.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527