TCU YAVIFUTIA UDAHILI VYUO 12 TANZANIA


Maafisa wa TCU wakiongozwa na Katibu Mtendaji Prof Charles Kihampa.

Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imeendelea kutoa adhabu ya kuvifutia udahili vyuo mbalimbali nchini ambapo mpaka sasa tume hiyo imeshavifutia udahili vyuo 12 nchini na kuvitaka vyuo husika kufanyia marekebisho baadhi ya maelekezo waliyopewa.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Charles Kihampa amesema katika kipindi cha mwaka 2018/2019 tume hiyo imefungia vyuo vikuu 10 na kutangaza vyuo vipya 2 walivyofungia.

"Mpaka kufikia sasa vyuo vikuu 12 tumevifutia udahili na haviruhusiwi kudahili wanafunzi wapya mpaka pale watakapomilisha baadhi ya maelekezo ambayo tume imewapa na katika mda waliopewa na kuhakikisha kuendelea kuvifanyia ukaguzi wa mara kwa mara."

Katika taarifa yake Katibu Mtendaji wa TCU Charles Kihampa amesema pia imefuta udahili baadhi ya masomo katika vyuo vya IMTU, Chuo cha
Mtakatifu James, Chuo cha Stefano Moshi pamoja na Chuo cha Sebastian Koloa.

"Tume pia imeendelea kusitisha udahili wa vyuo vikuu viwili ni chuo kikuu kishiriki cha Afya Ifakara Morogoro, na Chuo cha Mtakatifu Mihayo Morogoro mpaka tume itakapojiridhisha," ameongeza Prof Kihampa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527