RAIS MAGUFULI AZINDUA MAGARI YA JESHI KUBEBEA KOROSHO


Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo akiwa na Rais Magufuli.

Sakata la zao korosho limeingia kwenye sura mpya baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo kufika makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa ajili ya kukagua magari yatakayotumika kwenye ubebaji wa korosho.

Akizungumza alipotembelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Mkuu wa Majeshi nchini, Venance Mabeyo amesema alipokea maagizo kutoka kwa kiongozi huyo wa nchi ili kuanza utekelezaji.

Mabeyo amesema “nakumbuka ulinipigia simu ukaniuliza kama tunauwezo wa kusomba au kununua korosho kutoka kwa wakulima, kwa mikoa ambayo inalima korosho na mimi nilimuelekeza kwa Mkuu wa Jeshi la Taifa nchini ili kuyandaa magari, na kusaidia kubangua korosho kwa hiyo tuko tayari kwa zoezi hilo.”

Mapema leo akikagua magari hayo Rais Magufuli amesema endapo serikali itashindwa kununua zao hilo serikali itakuja na operesheni korosho ili kuwaokoa wakulima.

“Tumejifunza wametupa akili mapema wamechelewa na korosho zetu tutaziuza, na msimamo huu pia utaendelea kwenye mazao mengine kwa wale watakaotaka kuchezea wakulima, lazima tujipange kikamilifu.”

Wakati huohuo kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina nchini imetangazaa kukitwaa kiwanda cha kuchakata korosho Mkoani Lindi (BUKO) kwa madai kushindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527