MKUU WA MKOA WA TABORA AMSUKUMIA NDANI AFISA MANUNUZI


Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri na Afisa Manunuzi Wilaya ya Sikonge, Silvanus Ndilabika.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Aggrey Mwanri ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani kaimu Afisa Manunuzi Wilaya ya Sikonge, Silvanus Ndilabika kutokana na kuwepo kwa dalili za ufisadi katika ujenzi vituo viwili vya afya.

Mwanri amechukua hatua hizo leo kwenye ziara yake wilayani humo ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya afya mbalimbali ambapo katika ujenzi wa kituo cha afya cha Kitunda imeonekana kuna ufisadi hivyo kupelekea mradi huo kutokamilika kwa wakati.

''Unaona taratibu za manunuzi hazijafuatwa halafu unaongea kwenye kikao changu kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama unaniambia sikiliza unatoa wapi nguvu hiyo hebu mkamateni huyo'', alisema Mwanri.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amewataka watumishi wa umma mkoani humo kuhakikisha wanabaini kasoro za miradi mapema kabla ya kusubiri yeye ndio akabiani hilo.

Mwanri anafanya ziara yake katika wilaya za mkoa huo kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya afya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527