BALOZI WA JAPAN ATEMBELEA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA


Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi alipotembelea ofisini kwake kabla hajaenda kukagua eneo ambapo zitajengwa ofisi za ubalozi wa Japan
Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto akiangalia mchoro wa ramani wa eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Ubalozi wa Japan Mkoani Dodoma baada ya kufanya ziara ya kukagua.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi akisisitiza jambo kwa Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto baada ya kufanya ziara ya kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi akiwa na Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto na baadhi ya viongozi wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi akizungumza na Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto baada ya kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma
Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto atoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi walipotembelea eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani 
Hilo ndio eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma
Baada ya kumaliza kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma Balozi wa Japan akiwa na Mkurugenzi wanaelekea katika kupanda gari 
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhia maji kwenye eneo hilo ambalo litakuwa na ujazo wa lita milioni moja.
Fundi anayejenga tanki kubwa la kuhifadhia maji kwenye eneo hilo ambalo litakuwa na ujazo wa lita milioni moja akitoa maelezo kwa Balozi wa Japan nchini Sinichi Goto kwa upande wa (kushoto) Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi akisikiliza kwa umakini.
Balozi wa Japan nchini Sinichi Goto akisaini kitabu cha wageni baada ya kumaliza kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma.

PICHA NA ALEX SONNA WA FULLSHANGWEBLOG

...................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto ametembelea eneo la mji wa Serikali kwa dhumuni la kuona maendeleo ya ujenzi wa miondombinu pamoja na kiwanja kilichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za ubalozi huo, jiji Dodoma.

Akizungumzia ziara ya balozi huyo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwini Kunambi, amesema kuwa zaidi ya mabalozi 20 wameshafika Dodoma kujionea maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zao.

“Balozi wa Japan amekuja kuona eneo ambalo ubalozi wa nchi yake utajengwa, pamoja hilo amekuja miondombinu ambayo inaendelea kujengwa," ameeleza Kunambi

Aidha Kunambi amesema kuwa Jiji la Dodoma lipo kwenye ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhia maji kwenye eneo hilo ambalo litakuwa na ujazo wa lita milioni moja.

Hata hivyo amesema kuwa ujenzi huo utakamilika Januari mwakani kwa lengo la kusambaza maji kwenye eneo la mji wa serikali kabla ya kufikiwa na miundombinu ya Mamlaka ya Majisafi ya Jiji la Dodoma (DUWASA)

Mkurugenzi huyo aliwahakikishia watumishi wanaohamia Dodoma kuwa huduma muhimu zinapatikana ikiwemo maji kwani wanazalisha lita 61,000 kwa siku huku mahitaji yakiwa lita 48,000.

Kwa upande mwingine Kunambi amesema kuwa bado wanaendelea na utatuzi wa migogoro ya ardhi ambayo imeirithi kutoka Mamlaka ya ustawishaji Makao Makuu (CDA).

“Tunaendelea na utatuzi wa migogoro ya ardhi ndani ya Jiji la Dodoma, naikumbukwe masuala ya ardhi yalikuwa chini ya CDA. Rais alipovunja CDA, sasa masuala ya ardhi yote yanashughurikiwa na Jiji la Dodoma, tunahakikisha tunamaliza migogoro hii ns kuwa historia,” amesema Kunambi.

Alieleza ili kuhakikisha migogoro hiyo inamalizika walianzisha mpango wa kufanya ziara katika kata zenye migogoro ya ardhi na kuitatua kwenye eneo husika ili kujionea uhalisia.

AIizitaja kata hizo ni Kikuyu Kaskazini, kikuyu kusini, Ipagala na Dodoma Makulu ambapo sasa migogoro imepungua.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post